Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Shadrak Mwakalila.akiwahutubia
wahitimu wakati wa Mahafali ya Tisa ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu
Nyerere siku ya tarehe 22 Novemba, 2014 jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Mhe. Angellah Kairuki (kushoto)
akiwahutubia wahitimu wakati wa Mahafali ya Tisa ya Chuo cha Kumbukumbu
ya Mwalimu Nyerere siku ya tarehe 22 Novemba, 2014 jijini Dar es
Salaam.
Baadhi ya wahitimu wa ngazi mbalimbali wakifuatlia hotuba toka kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Mhe. Angellah Kairuki wakati wa Mahafali ya Tisa ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere siku ya tarehe 22 Novemba, 2014 jijini Dar es Salaam
SERIKALI
imekuwa ikifanya jitihada za dhati katika kukabiliana na changamoto ya
kushuka kwa kiwango cha wahitimu wa kidato cha Nne na Sita katika
kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Kauli
hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Mhe.
Angellah Kairuki wakati wa Mahafali ya Tisa ya Chuo cha Kumbukumbu ya
Mwalimu Nyerere yaliyofanyika 22 Novemba, mwaka huu jijini Dar es
Salaam.
Mhe.
Kairuki aliwaeleza wahitimu hao kuwa, katika taarifa iliyotolewa na
Mkuu wa Chuo hicho inaonyesha kuwa idadi ya wahitimu imepungua kutoka
wahitimu 919 mwaka jana, hadi kufikia 689 mwaka huu, hali iiyochangiwa
na kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa wahitimu wa vidato hivyo vya Sita
na Nne.
Alieleza
kuwa, Serikali imefanya juhudi za kukabiliana na tatizo hilo kwa
kuanzisha Mikakati mbalimbali ikiwemo; Mpango wa Elimu ya Shule za
Msingi, Mpango wa Elimu ya Sekondari, Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya
Ufundi wa miaka mitano (2013/14-2017/18) pamoja na Mpango wa Matokeo
Makubwa Sasa “Big Results Now” (BRN).
Mhe.
Kairuki alibainisha kuwa, jitihada hizo zinaonyesha dhamira ya dhati ya
serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutatua ufumbuzi wa
changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu nchini.
“Ni
matumaini yangu kwamba, juhudi hii za serikali zinazaa matunda na
zimeanza kujionyesha kwa kupanda kwa kiwango cha ufaulu katika shule
zetu za sekondari nchini, hivyo ni dhahiri kuwa kasi ya udahili katika
vyuo vyetu itaongezeka halikadhalika na idadi ya wahitimu kwa siku
zijazo”, alisema Kairuki.
Aliwaasa
wahitimu wa chuo hicho na kuwataka kujiepusha na tabia hatarishi
zinazoweza kuwaharibia maisha yao zikiwemo tabia za ngono zembe pamoja
na utumiaji wa madawa ya kulevya.
“Ninawasihi
mjiepushe na starehe na tamaa zinazoweza kuwaletea matatizo makubwa,
tumieni vizuri elimu mliyoipata chuoni hapa kwa kutunza afya zenu,
kuzingatia maadili mema na kutawala nafsi zenu, lakini pia jiendelezeni
kitaaluma, msiridhike na viwango vya elimu mlivyonavyo”, aliongeza
Kairuki.
Naye
Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Shadrak Mwakalila alisema kuwa katika
kutekeleza matakwa ya kisheria, hususani Sheria Namba Sita ya mwaka 2005
ya Chuo hicho, chuo kiliweza kukamilisha ujenzi wa Tawi la chuo cha
Mwalimu Nyerere upande wa Zanzibar ambapo jengo moja lenye ghorofa Nne
katika eneo la Bububu mjini humo lilizinduliwa rasmi na Rais wa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein siku ya tarehe 18
Mei, 2013 na limeweza kutoa fursa ya kuendesha mafunzo ya ngazi ya
Cheti katika Kazi za Vijana na hivi sasa chuo kinatarajia kuongeza
programu nyingine za mafunzo katika tawi hilo.
Akizitaja
baadhi ya changamoto zinazoikabili chuo hicho alisema kuwa, kuna uhaba
mkubwa wa hosteli kwa upande wa chuo cha Kivukoni pamoja na Tawi lake la
Zanzibar, pia kumekuwepo na ufinyu wa bajeti ambao unaathiri
utekelezaji wa majukumu ya chuo hicho, na matatizo mengine ni mmomonyoko
wa ardhi katika fukwe za Bahari ya Hindi unaohatarisha kuangusha baadhi
ya majengo ya chuo hicho.
Katika
mahafali hayo, jumla ya wahitimu 689 wakiwemo wanawake 400 sawa na
asilimia 58.1 na wanawaume 289 sawa na asilimia 41.9 walihitimu elimu
yao katika ngazi za Cheti, Stashahada ya Kawaida pamoja na Shahada ya
Kwanza
Post a Comment