PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MREMA AWALIPUA KNCU BUNGENI DODOMA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
    Na Salome Kitomari, Dodoma MBUNGE wa Vunjo (TLP), Agustino Mrema, juzi aliwalipua Bungeni viongozi wa Chama kikuu cha ushirika Mkoa...
 

 

Na Salome Kitomari, Dodoma

MBUNGE wa Vunjo (TLP), Agustino Mrema, juzi aliwalipua Bungeni
viongozi wa Chama kikuu cha ushirika Mkoani Kilimanjaro (KNCU) kwa
madai kuwa wanatafuna fedha za wakulima sambamba na kuuza mali za
ushirika kinyemela.

Mrema alitaka mwongozo wa Waziri kwa wakulima wa kahawa katika
kuwashughulikia viongozi wa KNCU kwa kuwa sheria inayosema wahusika
wanaohusika watakamatwa na kufungwa lakini haitekelezwi.

Alisema ripoti inaonyesha ubadhirifu wa fedha wa kutisha ikiwamo
uamuzi wa Mwenyekiti wa KNCU, Maynard Swai, kuitisha Mkutano mkuu
Maalum wa wanachama na kupendekeza kuuzwa kwa shamba la Garagagua
lenye ukubwa wa ekari 3,429 mali ya chama hicho likiwa na mali nyingi.

Mrema alisema pia KNCU inauza mali za kiwanda cha kukoboa kahawa cha
TCCCo, lengo likiwa ni kupata fedha za kulipa deni la Benki ya CRDB
ambalo hadi kufikia Juni 2012 limefikia Shilingi Bilioni 4.


Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christoper Chiza, alisema
viongozi na wanachama wa Ushirika wanapaswa kuelewa kuwa vyama vya
ushirika siyo idara za serikali na kwamba wanapokuwa ndani ya ushirika
na watu wanafanya madudu na kuogopa kuchukua hatua a kusubiri kauli ya
Waziri siyo sahihi.

"Mambo mengine yanakuja kwangu kwa kuchelewa sana, sikujua kama mnauza
hayo mashamba, TCCCo walianza kufanya utaratibu wa kuuza, mali ni yao
siyo ya msajili wa Hazina, wamekubaliana wao mimi sijajua, tumetuma
mrajisi wa vyama akakague na kuchukua hatua," alisema.

Alisema kwa sasa mali za TCCCo baada ya kuona kuna ujanja ujanja
aliandika barua kusimamisha mchakato huo na kwamba suala la kuuza
shamba la Garagagua halitauzwa kwa sababu hakuna hakika kama shamba ni
la wakulima au la serikali.

"Kuuzwa kwa shamba nimejua siku tatu zilizopita nimeagiza hawatauza
hadi tujiridhishe mlipewa na serikali au shamba ni lenu.Naomba
mnapofikia mahali mmeshindwana mtoe taarifa haraka tuchukue hatua,"
alisema.

Chiza alisema ukaguzi wa KNCU umekamilika na Mrajisi atatumia rungu
lake kiserikali kuchukua hatua pale ambako wanaushirika wenyewe
watasema wasaidiwe kiserikali.

"Nakuhakikishia tutachukua hatua," alisisitiza na hivyo Mrema
kukubaliana na hoja na kurudisha shilingi na hoja kupita.

 



About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top