PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: HAMISI KIGWANGALA AIWEZESHA KWAYA YA MSIFUNI JUMLA YA SHILINGI MILLIONI 14!!!!
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mheshimiwa Hamissi Kigwangalla akivishwa vazi la heshima la kimaasai kabla ya kuingia kanisani ili kufanya uzinduzi wa DVD ya kwaya ya ...


Mheshimiwa Hamissi Kigwangalla akivishwa vazi la heshima la kimaasai kabla ya kuingia kanisani ili kufanya uzinduzi wa DVD ya kwaya ya MSIFUNI ya kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania usharika wa Olorieni  jijini A rusha mapema leo

akielekea katika ofisi za kanisa hilo mara baada ya kufanya uzinduzi wa DVD ya kwaya ya MSIFUNU kanisani hapo mapema leo

 Mkuu wa mkoa wa Wilaya ya Arumeru Nyirembe Munassa (aliyevaa vazi la rubega nyekundu) aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Arusha aliyehamishiwa mkoa wa Mwanza Magessa Mulongo akilakiwa na waratibu wa uzinduzi wa DVD ya kwaya ya MSIFUNI ya kanisa la mtaa wa MARA usharika wa olorieni jimbo la kaskazini kati jijini Arusha mapema leo 30/11/2014 kanisani hapo

Mchungaji kiongozi wa kanisa la mtaa wa MARA usharika wa Olorieni kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania jimbo la kati akitabaruku DVD za kwaya za msifuni iliyozinduliwa leo na mgeni rasmi mbunge wa Nzega mheshimiwa Hamisi Kigwangalla

Mbunge wa jimbo la Nzega na mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge TAMISEMI Hamissi Kigwangalla akihojiwa na mwandishi wa habari wa gazeti la mwananchi jijini Arusha MUSSA JUMA mara baada ya kufanya uzinduzi wa DVD ya kwaya ya MSIFUNI  na haramee ya kanisa la KKKT olorieni lililopo jijini Arusha


 Mheshimiwa Hamissi Kigwangalla akiwahutubia waumini wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania usharika wa Olorieni na kuwaasa kuthamini  amani umoja na mshikamano ili kwa pamoja kushirikiana vema kupata fursa ya kuabudu na kuheshimu maoni na mtazamo wa kila mmoja
Hapa mgeni Rasmi Hamisi Kigwangalla akiwasihi waumini hao hawapo pichani juu ya kudumisha amani na Upendo miongoni mwa watu wa itikadi na dini tofauti ili uhuru wa kuabudu udumishwe nchini

akiwashukuru wanakwaya wa kwaya ya MSIFUNI  kwa kumpa heshima ya kipeke kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa DVD yao
Mgeni rasmi na mbunge wa jimbo la Nzega Hamissi Kigwangalla akikaribishwa na waratibu wa uzinduzi wa DVD ya kwaya ya MSIFUNI ya kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania Usharika wa Olorieni jijini Arusha mapema leo ambapo yeye binafsi alichangia kiasi cha shillingi millioni sita za kitanzania
Mchungaji kiongozi wa kanisa la mtaa wa Mara usharika wa Olorieni jimbo la kaskazini kati kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania mchungaji MKEMWA akizungumza na baadhi ya waandishi wa Habari waliohudhuria uzinduzi wa DVD ya kwaya ya Msifuni mapema leo  
Jumla ya shilingi milioni 14 zimechangwa katika hatambee ya  uzinduzi wa albamu na DVD ya kwaya ya MSIFUNI ya kanisa la kinjili la kilutheri Tanzania usharika wa Olorieni jimbo la kaskazni Kati jijini Arusha. 
 
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Dokta Hamisi Kigwangala ambaye ni mbunge wa jimbo la Nzega na mwenyekiti wa kamati ya bunge  inayosimamia TAMISEMI amewaasa wanakwaya wa kwaya ya MSIFUNI kuendelea kumtumikia Mungu kwa kuimba na kusifu ili amani upendo na ushirikiano miongoni mwa watanzania udumu milele.

 Akizindua DVD ya kwaya ya MSIFUNI ya kanisa la KKT olorieni mapema leo amesema kuwa kazi ya kumtumikia Mungu ni ya kipekee kwani inalenga  kuwajenga watu kiimani, kuleta ushirikiano na amani nchini Tanzania  ambapo
katika uzinduzi huo  aliwezesha kupatikana kwa jumla ya shilingi milioni 14
ambapo mchnganuo wa fedha hizo
fedha taslimu 2,965,400
ahadi ni 7,120,000/=Tshs
hundi 4,400,000/=Tshs
kati ya fedha hizo mheshimiwa Kigwangala alichangia jumla ya shilingi millionsita, ofisis ya mkuu wa m,koa wa Arusha shilingi millioni tano na mkuu wa wilaya ya Arumeru alichangia shilingi millioni moja na nusu na waumini mbalimbali walichangia sehemu iliyobaki

Hata hivyo hakusita kuelezea sakata la escrow account ambapo amemshukuru Mungu kwani limemalizika vema pasi na kuwagawa wananchi wa Tanzania  ambapo alisema wameazimia kuwa mawziri wawili lazima waondolewe, katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini avuliwe wadhifa wake na mwanasheria mkuu wa serikali avuliwe nyadhifa zake na kufikishwa katika vyombo vya sheria na ikithibitika wametenda kosa wafilisiwe mali zao ili zirejeshwe  kwa umma
amesisitiza kuwa haiwezekani mtu aibie watanzania halafu aachiwe huru na kuendelea na maisha yake pasi na kushtakiwa kwani itakuwa haijawasaidia watanzania.

alipoulizwa na wanahabari ni kwa nini hawajataka kumuajibisha waziri mkuu alisema kuwa katika ishu hii ya esrow account hakushiriki moja kwa moja kushinikiza au kupanga ubadhirifu huo wa fedha za uma na hivyo bunge kuazimia kutomchukulia hatua yoyote 

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top