PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MAMBA AMTAFUNA MTOTO WA DARASA LA SITA HUKO KATAVI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  MWANAFUNZI wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Ugalla, Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi,  Yohana Ramadh...

 


MWANAFUNZI wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Ugalla, Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi,  Yohana Ramadhani (14), ameliwa na Mamba wakati akioga na wenzake katika mto Ugalla.

Kwa mujibu wa Diwani wa Kata ya Ugalla, Mohamed Asenga, tukio hilo lilitokea Oktoba 18 mwaka huu, saa 11:00 jioni katika mto huo. Alisema siku  hiyo, marehemu akiwa na  watoto wenzake kamailivyo kawaida yake, alikwenda kwenye mto huu kwa lengo la kuogelea.

Asenga alisema kuwa, wakati watoto hao wakiendelea kuogelea, alitokea mama mmoja aliyefika mtoni hapo kwa ajili ya kuteka maji, ambapo akiwa anaendelea, alimwona mamba kando ya mto akiwavizia watoto hao pasipo wao kujua. Kwamba, mama yule aliwaambia waache kuogelea na watoke haraka ndani ya mto kwani amemwona mamba akiwa pembeni akiwavizia.

“Watoto hao walitoka ndani ya mto lakini wakati wakiondoka mamba huyo aliyekuwa pembezoni mwa mto, alimkamata Yohane na kuingia naye mtoni tena,” alisema na kuongeza kwamba zilipiga yowe kuomba msaada ambapo wananchi walijitokeza japo hawakufanikiwa kumuokoa. 

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top