MWANANCHI
Mbio za urais ndani ya CCM zimechukua sura mpya baada ya aliyekua
Katibu mkuu wa CCM Yusuph Makamba kutangaza rasmi kumuunga mkono mtoto
wake January Makamba kwa sababu anaamini mwanaye ana uwezo.
“Mbali ya kwamba January ni mwanangu,lakini najua ana uwezo na
anajua shida za Watanzania kwa kuwa alikua msaidizi wa Jakaya Kikwete
ambaye walizunguka naye Tanzania na dunia nzima”alisema Makamba
Mzee Makamba alisema ameamua kufunguka kuhusu kumuunga mkono mwanaye
baada ya watu wengi kumhoji kuhusu nani anayefaha kuongoza Taifa mara
baada ya rais wa sasa kuondoka madarakani.
Alisema pamoja na mwanaye kutangaza nia hiyo akiwa nje ya nchi
alishangazwa na maamuzi yake kwani hakuwahi kumpa taarifa lakini ameamua
kumsapoti akiamini anaweza kuiongoza nchi licha ya umri wake kuwa bado
mdogo.
MWANANCHI
Jeshi la polisi limesitisha mafunzo kwa askari132 waliokua katika
chuo cha Polisi Zanzibar kwa kile kinachodaiwa kuwa ni sababu za kiafya.
Taarifa zilizopatikana kutoka vyanzo mbalimbali vya habari chuoni
hapo kati ya askari hao walioondolewa chuoni hapo mwishoni mwa juma
lililopita mmoja wao Koplo Abdalah alifariki dunia akiwa chumbani
kutokana na shinikizo la damu baada ya kupata taarifa ya kuondolewa
chuoni.
Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdani Makame alisema amewasitishia
kufanya mafunzo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kiafya lakini
ajira zao zitaendelea kama kawaida na wataendelea na kazi zao.
Alisema askari aliyefariki alikua akisumbuliwa na kisukari kwa muda
mrefu na alifariki wakati wenzake wakijiandaa kwa mazoezi ya asubui
chuoni hapo.
MWANANCHI
Mahabusu Daniel Alfred wa kituo cha urafiki Dar es salaam amefariki
dunia kwa madai ya kupigwa na baadhi ya askari wa kituo hicho.
Kamanda wa Polisi Kinondoni Camilius Wambura alithibitisha kutokea
kwa kifo hicho huku akisema kijana huyo alikua akifanya fujo na kuwapiga
wenzake walipokua katika chumba cha mahabusu.
Wambura alisema ripoti ya daktari aliyepokea mwili wake ilionyesha
mahabusu huyo alikua mgonjwa lakini shuhuda wa tukio hilo alisema
alikwenda kituo cha polisi na kukuta askari wakimpiga ndugu yake.
NIPASHE
Ripoti ya Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali imeonyesha
kuwa serikali imeendelea kutoa misamaha mikubwa ya kodi ambayo ni
asilimia kumi ya bajeti ya mwaka 2012/13.
Kwa mujibu wa ripoti ya ukaguzi wa fedha za Serikali kuu kwa mwaka
huo iliyowasilishwa na CAG inaonyesha kuwa misamaha ya kodi ni zaidi ya
bilioni1 sawa na asilimia kumi ya bajeti ya mwaka huo ya zaidi ya
shilingi trilion15.
Wakati Serikali ikiendelea kutoa misamaha ya kodi kumekuwepo na
malalamiko kwamba misamaha hiyo ipunguzwe ili Serikali ipate mapato
zaidi kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo na kutoa huduma muhimu
kwa wananchi.
MWANANCHI
Ndoa ya Shirikisho la soka Tanzania na Kampuni ya bia ya TBL iko
shakani baada ya kampuni hiyo kutishia kusitisha udhamini wake wa zaidi
ya bilioni17 kutokana na kubaini matumizi mabaya ya mamilioni ya fedha.
TBL na TFF zilisaini mkataba wa udhamini wa timu ya Taifa ‘Taifa
Stars’ mwaka 2012 ukiwa na thamani ya dola za kimarekani milioni10 ukiwa
ni wa miaka mitano na huu ni mwaka wa pili.
Habari ambazo gazeti hili zimepata ni kwamba ufisadi huo umegundulika
kwenye akaunti ya fedha za udhamini wakati wa ukaguzi wa robo nne za
mwisho katika kipindi cha udhamini kilichoishia Mei2014.
Ukaguzi huo ulionyesha kulikua na matumizi ya zaidi ya bilioni1.4
ambao ulifanywa bila kuheshimu masharti ya mkataba na kwa kukiuka kanuni
za fedha za TFF.
TANZANIADAIMA
Wakati mtoto wa Mbunge wa Temeke Sitti Mtemvu akiandamwa na kashfa za
kughushi umri baada ya kushinda taji la Miss Tanzania, baba yake mzazi
Abbas Mtemvu ameibuka na kudai sakata hilo ni vita ya kisiasa
inayoratibiwa na wapinzani wake ndani ya CCM.
Mtemvu alisema inasikitisha watu wanaolitaka jimbo hilo kumwandama
kwa kashfa binti yake kwa maslahi yao binafsi ya kisiasa hivyo ni vyema
waende kwa hoja na si kupakana matope.
Alisema amesikitishwa na kashfa hizo kwa binti yake na kudai hayo ni
matusi kisa siasa na maneno hayo yamekua yakienezwa na mjumbe wa NEC
ambaye hakutaka kumtaja jina lake.
MWANANCHI
Baadhi ya wakunga wa jadi Wilayani Kiteto huvaa mikononi mifuko ya
plastiki maarufu kama rambo ili kuwahudumia kina mama wakati wa
kujifungua.
Awali wakunga hawa ambao hufanya kazi bila malipo yoyote walikua
wakizalisha wajawazito bila kuvaa chochote lakini walianza kutumia aina
hiyo ya kinga baada ya wenzao wawili kuambukizwa Ukimwi.
Mmoja wa wakunga hao Rosemary Loshiye alisema walikua wakiwazalisha
wakinamama bila kuvaa aina yoyote ya kinga na kusababisha wenzao wawili
kuambukizwa Ukimwi kutokana na kuwepo na ukosefu wa vifaa bora kwa ajili
ya uzazi.
Alisema wanapouliza sababu za kutopatiwa vifaa vya kuwahudumia
wajawazito wanaelezwa kwamba hawatambuliwi na hawapaswi kusaidiwa
kuzalisha.
MAGAZETI YA TANZANIA KWA UFUPI SIKU YA LEO
Title: MAGAZETI YA TANZANIA KWA UFUPI SIKU YA LEO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
MWANANCHI Mbio za urais ndani ya CCM zimechukua sura mpya baada ya aliyekua Katibu mkuu wa CCM Yusuph Makamba kutangaza rasmi kumuunga ...
Post a Comment