PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MAGAZETI YA TANZANIA KWA UFUPI SIKU YA LEO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
MWANANCHI Mbio za urais ndani ya CCM zimechukua sura mpya baada ya aliyekua Katibu mkuu wa CCM Yusuph Makamba kutangaza rasmi kumuunga ...
MWANANCHI
Mbio za urais ndani ya CCM zimechukua sura mpya baada ya aliyekua Katibu mkuu wa CCM Yusuph Makamba kutangaza rasmi kumuunga mkono mtoto wake January Makamba kwa sababu anaamini mwanaye ana uwezo.
“Mbali ya kwamba January ni mwanangu,lakini najua ana uwezo na  anajua shida za Watanzania kwa kuwa alikua msaidizi wa Jakaya Kikwete ambaye walizunguka naye Tanzania na dunia nzima”alisema Makamba
Mzee Makamba alisema ameamua kufunguka kuhusu kumuunga mkono mwanaye baada ya watu wengi kumhoji kuhusu nani anayefaha kuongoza Taifa mara baada ya rais wa sasa kuondoka madarakani.
Alisema pamoja na mwanaye kutangaza nia hiyo akiwa nje ya nchi alishangazwa na maamuzi yake kwani hakuwahi kumpa taarifa lakini ameamua kumsapoti akiamini anaweza kuiongoza nchi licha ya umri wake kuwa bado mdogo.
MWANANCHI
Jeshi la polisi limesitisha mafunzo kwa askari132 waliokua katika chuo cha Polisi Zanzibar kwa kile kinachodaiwa kuwa ni sababu za kiafya.
Taarifa zilizopatikana kutoka vyanzo mbalimbali vya habari chuoni hapo kati ya askari hao walioondolewa chuoni hapo mwishoni mwa juma lililopita mmoja wao Koplo Abdalah alifariki dunia akiwa chumbani kutokana na shinikizo la damu baada ya kupata taarifa ya kuondolewa chuoni.
Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdani Makame alisema amewasitishia kufanya mafunzo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kiafya lakini ajira zao zitaendelea kama kawaida na wataendelea na kazi zao.
Alisema askari aliyefariki alikua akisumbuliwa na kisukari kwa muda mrefu na alifariki wakati wenzake wakijiandaa kwa mazoezi ya asubui chuoni hapo.
MWANANCHI
Mahabusu Daniel Alfred  wa kituo cha urafiki Dar es salaam amefariki dunia kwa madai ya kupigwa na baadhi ya askari wa kituo hicho.
Kamanda wa Polisi Kinondoni Camilius Wambura alithibitisha kutokea kwa kifo hicho huku akisema kijana huyo alikua akifanya fujo na kuwapiga wenzake walipokua katika chumba cha mahabusu.
Wambura alisema ripoti ya daktari aliyepokea mwili wake ilionyesha mahabusu huyo alikua mgonjwa lakini shuhuda wa tukio hilo alisema alikwenda kituo cha polisi na kukuta askari wakimpiga ndugu yake.
NIPASHE
Ripoti ya Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali  imeonyesha kuwa serikali  imeendelea kutoa misamaha mikubwa ya kodi ambayo ni asilimia kumi ya bajeti ya mwaka 2012/13.
Kwa mujibu wa ripoti ya ukaguzi wa fedha za Serikali kuu kwa mwaka huo iliyowasilishwa na CAG inaonyesha kuwa misamaha ya kodi ni zaidi ya bilioni1 sawa na asilimia kumi ya bajeti ya mwaka huo ya zaidi ya shilingi trilion15.
Wakati Serikali ikiendelea kutoa misamaha ya kodi kumekuwepo na malalamiko kwamba misamaha hiyo ipunguzwe ili Serikali ipate mapato zaidi kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo na kutoa huduma muhimu kwa wananchi.
MWANANCHI
Ndoa ya Shirikisho la soka Tanzania na Kampuni ya bia ya TBL iko shakani baada ya kampuni hiyo kutishia kusitisha udhamini wake wa zaidi ya bilioni17 kutokana na kubaini matumizi mabaya ya mamilioni ya fedha.
TBL na TFF zilisaini mkataba wa udhamini wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ mwaka 2012 ukiwa na thamani ya dola za kimarekani milioni10 ukiwa ni wa miaka mitano na huu ni mwaka wa pili.
Habari ambazo gazeti hili zimepata ni kwamba ufisadi huo umegundulika kwenye akaunti ya fedha za udhamini wakati wa ukaguzi wa robo nne za mwisho katika kipindi cha udhamini kilichoishia Mei2014.
Ukaguzi huo ulionyesha kulikua na matumizi ya zaidi ya bilioni1.4 ambao ulifanywa bila kuheshimu masharti ya mkataba na kwa kukiuka kanuni za fedha za TFF.
TANZANIADAIMA
Wakati mtoto wa Mbunge wa Temeke Sitti Mtemvu akiandamwa na kashfa za kughushi umri baada ya kushinda taji la Miss Tanzania, baba yake mzazi Abbas Mtemvu ameibuka na kudai sakata hilo ni vita ya kisiasa inayoratibiwa na wapinzani wake ndani ya CCM.
Mtemvu alisema inasikitisha watu wanaolitaka jimbo hilo kumwandama kwa kashfa binti yake kwa maslahi yao binafsi ya kisiasa hivyo ni vyema waende kwa hoja na si kupakana matope.
Alisema amesikitishwa na kashfa hizo kwa binti yake na kudai hayo ni matusi kisa siasa na maneno hayo yamekua yakienezwa na mjumbe wa NEC ambaye hakutaka kumtaja jina lake.
MWANANCHI
Baadhi ya wakunga wa jadi Wilayani Kiteto huvaa mikononi mifuko ya plastiki maarufu kama rambo ili kuwahudumia kina mama wakati wa kujifungua.
Awali wakunga hawa ambao hufanya kazi bila malipo yoyote walikua wakizalisha wajawazito bila kuvaa chochote lakini walianza kutumia aina hiyo ya kinga baada ya wenzao wawili kuambukizwa Ukimwi.
Mmoja wa wakunga hao Rosemary Loshiye alisema walikua wakiwazalisha wakinamama bila kuvaa aina yoyote ya kinga na kusababisha wenzao wawili kuambukizwa Ukimwi kutokana na kuwepo na ukosefu wa vifaa bora kwa ajili ya uzazi.
Alisema wanapouliza sababu za kutopatiwa vifaa vya kuwahudumia wajawazito wanaelezwa kwamba hawatambuliwi na hawapaswi kusaidiwa kuzalisha.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top