Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye wakiwa katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Kalenga, Iringa Vijini, walipoanza ziara ya siku sita za kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 pamoja na kusikiliza kero za watu na kuzitafutia ufumbuzi.Katika mkutano huo Kinana aliitaka Serikali kuandaa utaratibu mzuri wa kuwatafutia soko la uhakika wakulima.
Kinana akivishwa vazi la kimila la wazee wa kabila la Wahehe ikiwa ni heshima kwake.
Kinana akiwa katika picha ya pamoja na wazee wa kimila baada ya kukabidhiwa mkuki.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipokea kadi ya Chadema kutoka Rehema Said, wakati alipopokea wanachama wapya kutoka Chadema kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Kalenga. Wanachama wapya 21 wa Chadema walijiunga na CCM
Kinana akionyesha kadi za Chadema alizokabidhiwa wakati wa mkutano huo
Kinana akiwa amekaa na Chifu Abdul Mkwawa pamoja na wazee wa kimila wa kabila la wahehe.
Kinana akipendeza na vazi la kihehe huku akiwa na mkuki mkononi.
Post a Comment