Mkuu
wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Kelvin Twissa
(katikati) akiongea na waandishi wa habari wakati akizindua huduma ya
LIPA KWA M PESA inayowawezesha wasambazaji wa huduma kupokea malipo ya
mauzo kwa njia ya M-pesa kutoka kwa wauzaji wajumla. Kampuni ya Chai
Bora na Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia wasamabzaji wake kampuni ya
Mahawi zimkuwa miongoni mwa wasambazaji wa awali kutumia huduma hiyo.
Wengine pichani ni Mwakilishi wa Mahawi Enterprises Joseph Mahawi na
kulia ni Meneja wa maendeleo ya Biashara wa Chai Bora Martin Ng’ethe.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na Chai Bora wakifuatilia mkutano wa
waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa huduma mpya ya LIPA KWA M
PESA inayowawezesha wasambazaji wa huduma kupokea malipo ya mauzo kwa
njia ya M-pesa kutoka kwa wauzaji wa jumla. Kampuni ya Chai Bora na
Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia wasamabzaji wake kampuni ya Mahawi
zimekuwa miongoni mwa wasambazaji wa awali kutumia huduma hiyo.
Vodacom
Tanzania imezindua huduma mpya ya M-PESA ijulikanayo kama "LIPA KWA
M-PESA – huduma hii mpya ya kisasa ni jumuishi ya mfumo wa malipo utakao
wezesha makampuni, mawakala wa jumla na rejareja na wafanyabiashara
wengine kulipia bidhaa zao kwa kutumia M-PESA.
Huduma
hii mpya imekuja ili kuboresha mazingira ya wafanyabiashara na
makampuni kwa kupanua mbinu za malipo kutoka kwa wafanyabiashara na
makampuni na wauzaji wa aina mbalimbali, sasa mawakala wa jumla na
rejareja wataweza kununua na kulipia bidhaaa zao kwa kutumia huduma hii
ya LIPA KWA M-PESA. Njia hii mpya ni ya haraka, salama na inampa mteja
wepesi zaidi wa kufanya biashara.
Akiongea
kwenye uzinduzi huo,Bw. Kelvin Twissa , Mkuu wa Kitengo cha Masoko na
Mawasiliano alisemasema, "Vodacom imekuwa ikiongeza thamani na kusaidia
kuboresha mbinu za ufanyaji wa biashara nchini kwa kuanzisha huduma
ambazo zitaleta mapinduzi kwa jumuiya ya wafanyabiashara, ili kuepuka
dhana za zamani za utendaji wa biashara. Huduma hii mpya ya LIPA KWA
M-PESA ni ya haraka, salamaj, urahisi na na inamrahisihia mteja
kuondokana na dhana ya kubeba hela nyingi kila saa ".
Wafanyabiashara
wengi nchini wanapendelea kutumia fedha (cash) wanapo nunua na kuuza
bidhaa zao, kwa sababu ni haraka. Hata hivyo nyakati hizi zinachangamoto
kubwa ukifanya biashara kwa aina hiyo hasa wale ambao wanakipato kiasi
na kikubwa cha fedha, aina hii ni tishio sana la kama wizi au hata
pengine kuhatarisha maisha ya mfanyabiashara. Lakini sio ujambazi tuu
hata pia ni gharama kubwa kusafirisha fedha na inagharimu muda mwingi wa
wafanyabiashara.
Huduma
hii mpya ya LIPA KWA M-PESA ni mapinduzi ya biashara, mfumo huu
umeunganishwa kwanye akaunti ya mteja ya M-PESA na pia inaweza
kuunganishwa na akaunti yako ya benki, ni kumuwezesha wafanyabiashara na
wauzaji kulipia bidhaa mara moja, na shughuli zote hii zinafanyika kwa
kupitia simu yako ya kiganjani. Mfumo huu mpya, unamuwezesha wakala
aliejisajili kuweza kuweka hadi kiasi cha Tsh milioni 50 katika
akauinti yake ya M-PESA tofauti na huduma ya M-PESA ya kawaida ambayo
ina kikomo ya shilingi milioni 5. Mawakala wakubwa wanaweza kushikilia
hadi Tsh bilioni 2 kwenye akaunti zao za M-Pesa. Hii ni fursa kubwa kwa
jumuiya ya wafanyabiashara katika Tanzania kuanza kufanya biashara bila
kua wanabeba noti kila saa.
Twissa
anaendelea kusema "Huduma hii mpya ni rahisi, salama, na ya kuaminika
na haina gharama yeyote. Sasa hivi mfanyabiashara haitaji tena kusafiri
kwenda kutuma fedha, njia hii ni ya haraka zaidi; Unabonyeza simu yako
tu marachache tu kuhitimisha biashara. Haihitaji makaratasi wala mtandao
wa Internet kwani imeunganishwa moja kwa moja na mtandao Vodacom GSM."
Jinsi
inavyofanya kazi ni rahisi sana, hakuna uwekezaji unao hitajika. Mara
baada ya wakala kujisajili anaweza kufanya shughuli yake yote katika
njia salama sana, mfumo unakupa taarifa ya mesegi (SMS) ya uthibitisho
wa kila muamala unaofanya baina ya wakala na kampuni na unaemtumia pesa
hizo na yeye anapata uthibitisho kua ni wewe unaemtumia wewe. Huduma
yote hii ni bure na sasa hivi zaidi ya wakala 24,000 nchini kote tayari
wamejiunga na huduma.
Akizungumza
katika uzinduzi huo,Bw Olestus Mwalongo, ambae ni muuzaji wa vifaa vya
ujenzi maeneo ya Buguruni, Dar es Salaam alisema "Nilitembelewa na
Vodacom miezi sita iliyopita kwa kushiriki katika zoezi la kuitumia
huduma hii, kabla ya kuletwa sokoni. Kwakweli faida ya huduma hii ni
kubwa sana, kwanza utaratibu wake ni rahisi sana kama tu kama unapiga
simu vile, pili unageuza maisha yako katika sura mpya. Zamani nilikua
napata tabu sana kusafirisha fedha kwaajili ya kufanya malipo. Sasa hivi
huduma hii imeniwezesha kupunguza gharama hizo na gharama zingine za
uendeshaji. Sasa hivi nafanya biashara yangu kwa nafasi zaidi na
nafarijika sana na huduma hii"
Kwa
upande wake, Bw. Joseph Mahawi ya Mahawi Enterprises, wakala wa
Serengeti Breweries alisema, 'Huduma hii ni salama na rahisi. Mimi sasa
wanaweza kupokea malipo kutoka kwa wauzaji mbalimbali na kulipia mambo
mengine huku nikipata taarifa za mahesabu yangu yote papo hapo. Huduma
hii mpya inamfumo taarifa sahihi na ni kipengele kikubwa sana kwangu.
Sasa naweza kusema biashara yangu inaenda vizuri sana na inaniruhusu
mimi kufanya shughuli zingine. Sasa hivi nina muda zaidi wa kufikiria
jinsi ya kukuza biashara yangu katika mwelekeo mpya. Zaidi ya hayo, siku
hizi sipangi foleni kabisa kwenye taasisi yeyote ya fedha kusubiri
kulipa wauzaji yangu. Sasa naweza kufanya hivyo nyumbani au mahali
popote kwa furaha tu'.
Kujisajili
na huduma ni rahisi; Wafanyabiashara na wauzaji unaweza kutembelea
wakala yeyote wa Vodacom alie karibu yako kwa maelezo zaidi na jinsi ya
kujisajili. Vodacom imetenga dawati maalum la huduma kwa mteja wa LIPA
KWA M-PESA.
Kwa maswali zaidi unaweza piga namaba 1500 muda wa wowote ndani ya masaa 24 siku zote za Juma bure.
Post a Comment