PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: HABARI MPYAAAAAAA: DOKTA KIGWANGALA ATANGAZA KUWANIA URAISI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mbunge wa Nzega, Dkt. Hamisi Kigwangala, akitangaza nia ya kugombea urais mbele ya waandishi wa habari kwenye hoteli ya Hyat...


Mbunge wa Nzega, Dkt. Hamisi Kigwangala, akitangaza nia ya kugombea urais mbele ya waandishi wa habari kwenye hoteli ya Hyatt Kilimanjaro Hotel jijini Dar es Salaam, Jumapili Septemba 7, 2014. Katika mkutano huo, Dkt. Kigwangala alifuatana na familia yake wakiwemo wazaziu wake wawili.

MBUNGE wa Nzega kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Dkt. Hamisi Kigwangala, ametangaza kugombea urais kwenye uchaguzi ujao wa mwak 2015.


Kigwangala ambaye ni daktari wa binadamu, alitangaza nia yake hiyo leo mbele ya waandishiw a habari kwenye hoteli ya Hyatt Kilimanjaro Kempisk jijini Dar es Salaam, na hivyo kupanua wigo wa wana CCM vijana kutangaza kuwania wadhifa huo mkubwa kabisa nchini.

Kijana mwingine kutoka chama hicho ambaye tayari alitangaza kuwania nafasi hiyo ni Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba.

Wengine wanaodaiwa kutaka kuwania nafasi hiyo ingawa bado hawajatangaza rasmi ni pamoja na Mawaziri wakuu wastaafu, Edward Lowasa, Frederick Sumaye, na waziri mkuu wa sasa Mizengo Pinda.

Katika orodha ya wanaotamani kuwania nafasi hiyo ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, Mwenyekiti wa Bunge Maalum lka Katiba, Samwel Sitta



Dokta Kigwangala akiwasilisha hoja katika bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania hivi karibuni

Mbunge wa jimbo la Nzega, mkoani Tabora, Dkt. Hamisi Kigwangala (Kushoto), akipokea sh. 500,000 kutoka kwa hasimu wake mkubwa kiasiasa, Hussein Bashe, ambazo alitoa kwa katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, (Wapili kushoto), kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya CCM tawi la Kipugala, jimbo la Nzega wakati wa ziara ya katibu mkuu wa CCM, Kinana hivi karibuni.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top