WAKAZI WA MOROMBO WALIA KUKOSA HUDUMA ZA JAMII
Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Wakazi wa Morombo Arusha wanaeleza kuwa wamekuwa wakikosa huduma za
maji kwa kipindi kirefu ikiwemo maji,shule na vituo vya afya kutokana
na maeneo mengi kujengwa hivyo kukosa miundombinu ya huduma hizo.
Mkazi wa Morombo Msovela Abeli anasema kuwa Serikali ingetakiwa
itangulize huduma za kijamii katika miji inayokua badala ya kuwaacha
wananchi watangulie kwenye miji hiyo kwanza ndio maana sasa hivi
hatuna huduma za kijamii zitapita wapi kila mahali pamejengwa,maeneo
ya wazi hakuna inakua vigumu kujenga shule na zahanati.
Mkazi wa eneo hilo ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini
anaeleza kuwa tatizo la ujenzi holela limesababishwa na uongozi mbovu
uliopo wamekua na tamaa wameruhusu kuuzwa kwa maeneo kiholela hata
maeneo ambayo yalikua ni soko zamani sasa ni makazi ya watu wamejenga
na kuishi humo.
Mfanyabiashara Michael Henry kipindi cha nyuma maeneo haya yalikua ni
soko lakini sasa yamejengwa ,hapa tunapofanyia shughuli tunaweza kuja
soko lijalo tukakuta pamejengwa.
Mfanyabiashara Laurian Baltazari anaeleza kuwa maeneo ya kufanyia
biashara yamekua finyu wanalazimika kupanga bidhaa zetu nje ya majengo
ya watu ,watu wenye eneo la biashara ni wafanyabiashara wa mnada wa
mbuzi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Morombo,Julius Kivuyo amekiri
kuwa ni kweli mji huo unakua kwa kasi ya ajabu na amekanusha madai ya
viongozi kuruhusu uuzwaji wa maeneo kiholela na kusema kuwa iwapo yuko
anayehusika afikishwe mahakamani.
Wachambuzi wa Masuala ya kijamii na kiuchumi jijini hapa Wameeleza
kuwa Mipango miji mibovu imekua janga kwa taifa kwasababu kuna maeneo
ambayo hayafikiki hata inapotokea majanga ya moto hupoteza maisha ya
watu na kuteketeza mali nyingi,maeneo hayo hata magari hayapiti
yametawaliwa na vichochoro maarufu kama njia za panya. Maeneo hayo yamekuwa yakisifika kwa kushambuliwa na magonjwa yamilipuko kama kipindu pindu kutokana na miundombinu mibovu kiasi chakutosafishika,Mfano maeneo ya Ungalimitedi,Ngarenaro,Matejo.
Post a Comment