zaidi ya wakazi elfu 12 wa maeneo ya Chamazi na Mbande jijini Dar es
Salaam, wameugomea mradi wa barabara ya njia sita iliyokuwa ipite katika
eneo lao kutokana na utata uliogubikwa na uwekaji wa mipaka ya kupita
barabara hiyo iliyopangwa kutoka Chamazi hadi Kisewe.
Wakazi hao wamesema kuwa
mipaka hiyo imewekwa kwenye upande mmoja kinyume na utaratibu unaotaka
uwekwe pande zote za mradi na kwamba hawatakubali mradi huohadi
watakapofafanuliwa juu ya utekelezaji wakesambamba na ulipwaji wa fidia.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo amesema wameshangazwa na ukakasi
uliojitokeza kuhusu barabara hiyo baada ya kuahidiwa kuwa ingetumia
ukubwa (upana) mkubwa ambao haujawahi kujenga hapa nchini barabara hiyo
itakuwa ni ya njia sita, yenye njia tatu zinakwenda na njia tatu
zinarudi na kuwa mradi huo uko chini ya Serikali ya Tanzania na Serikali
ya watu wa China kwa kiasi kikubwa inafadhili kutengeneza barabara hiyo
huku iukikadiriwa kuwa na upana wa mita 75 – 90, na itakuwa na urefu wa
Kilomita zisizopungua 14 tofauti na sasa ambapo wamepima upana wa mita
zaidi ya elfu moja (1,000).
“Tuliambiwa barabara itaanzia Ukonga Banana itapita pia Msongola,
Chamazi mpaka Mbagala lakini hii haihusiani na upanuzi wa barabara ya
Chamazi, ile inayotoka Mbagala rangi tatu kwenda kwenye uwanja wa timu
ya Bakhresa, Azam FC, na awamu ya kwanza itakuwa ni ya utambuzi, kuweka
alama ya eneo litakalochukuliwa na barabara, zoezi hili lingefanyika
baada ya sikukuu ya Eid na awamu ya pili itafuata ambapo itakuwa ni
uthamini wa nyumba na makazi wa wananchi watakaokuwemo ndani ya eneo
lililotambuliwa” kilisema chanzo chetu cha habari.
Aidha, wamesema fomu ya uthamini ambayo waliahidiwa kuwa itatumika fomu
No. 69 ambayo haihusishi majadiliano kati ya mnunuzi wa eneo na mwenye
eneo huku utata ukitokea kuhusu ardhi ya eneo hilo ambayo inathamani
kati ya shilingi 12,000 hadi 20,000 kwa (Square Meter) na kuwa maelezo hayo yalitolewa na Mthamini Mkuu wa Serikali.
Hata hivyo, wamesema “Inadaiwa kuwa huu mradi hauhusu barabara tu peke
yake bali pia na ujengaji wa 'bandari kavu', inadaiwa pia huu mradi
utakwenda mpaka Kisewe na kuwa sasa kuna wajanja wenye pesa kutokana na
kuwepo kwa mradi huu na wao wamejipenyeza (kupitia mgongo wa wenye
mradi) kuwahamisha watu ili waweze kununua maeneo kwa bei ya chini na
hivyo kupata maeneo ya uwekezaji ambayo yatakuwa kando kando mwa
barabara itakayojengwa”.
Awali imeripotiwa
kuwa wananchi hao wanaomba wasaidiwe mawazo juu ya kitu wanachotakiwa
kufanya ili wasipoteze haki zao za msingi na ukweli juu ya mradi huo
huku wakilaumu usiri taarifa hiyo ambayo imekuwa ikifanywa na serikali
kimya kimya bila kutangazwa hata kupitia vyombo vya habari.
Kwa upande wao Mwakilishi wa Baraza la Uhifadhi na usimamaizi wa
Mazingira NEMC (hakutaka jina lake litajwe), amesema mradi huo umelenga
kupunguza foleni za magari jijini Dar es Salaam na pia amewahakikishia
wananchi kuwa kupitia kwa baraza hilo watamaliza tofauti zilizopo baina
ya serikali na wakazi hao ili kuruhusu mradi kuendelea.
Post a Comment