PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: VIONGOZI WATAKIWA KUZIKUMBUKA SHULE WALIZOSOMEA PITIA hapa uone Shule waliyosoma Rais Joseph Kabila (wa DRC), Assah Mwambene yachakaa vibaya!
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  SHULE ya Sekondari ya Irambo inayomilikiwa na Chama Cha Mapindu...

 


SHULE ya Sekondari ya Irambo inayomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), iliyopo katika Wilaya ya Mbeya Vijijini inakabiliwa na tatizo la uchakavu wa miundombinu ya majengo hali inayotajwa kufanyiwa ukarabati ili kuendana na hadhi ya shule hiyo.
Shule hiyo inatwajwa kuongoza kutoa matokeo bora ya kitaaluma tangu kuanzishwa kwake, ambapo pia shule inatwajwa kuwa ndiyo waliyosoma viongozi maarufu Nchini Tanzania akiwemo Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assa Mwambene na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Irambo
Uchunguzi uliofanywa mkoani humo umebaini kuwa licha ya viongozi hao kusoma shuleni hapo, ufaulu wa shule hiyo umeshuka kwa kiwango kikubwa tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Makamu Mkuu wa shule hiyo, Aliko Mwanjala, amebainisha kuwa shule hiyo haina miundombinu ya kutosha licha ya kuwa na uhaba wa vifaa vya kufundishia huku akisema hali ya majengo ya shule hiyo kuwa sio rafiki.
Amesema awali shule hiyo ilikuwa ni shule ya mfano kitaaluma na kimalezi katika mkoa wa Mbeya na kuwa juhudi za kuinusuru na kuiinua kupitia kwa wadau mbalimbali wakiwemo wanafunzi waliowahi kusoma katika shule hiyo bado zinaendelea.
Mmoja wa watu waliowahi kusoma katika shule hiyo akiwemo Sambwee Shitambala, ambaye sasa ni Mwanasheria alikaririwa  akisema “Nitajitahidi kuwashirikisha wenzangu kuhusu hali hii naona majengo yamechakaa sana tofauti na tulivyokuwa tunasoma hapa kikiwemo jingo lenye chumba alichokuwa analala, Rais Kabila”.
Madarasa
Hata hivyo, amebainisha kuwa hapo awali shule hiyo ilikuwa inatumimiw ana watu wengi waliokuwa wakiwekwa kwa ajilio ya kufanya kazi kwenye idara nyeti za serikali na hivyo kuwataka watu wote waliosoma katika shule hiyo kwende shuleni hapo na kutoa misaada ya kuikarabati shule hiyo.
Darasa la Kabila
Taarifa za ndani kutoka kwa wanafunzi waliosoma katika shule hiyo waliopo katika maeneo mbalimbali nchini, wamesema kuwa mwanzoni mwa mwezi Septemba, 2014 wanakusudia kutoa misaada mbalimbali kwa ajili ya shule hiyo kupitia kikundi ambacho hawajapenda kukiweka wazi kilicho mbioni kusajiliwa kwa ajili ya shule hiyo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top