“Wakati
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisema kuwa suala la muundo wa serikali
lilitakiwa kupigiwa kura, Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samwel Sitta
anaendelea kuongoza Bunge kama mchakato ni mali yake binafsi. Baadhi ya
viongozi wa chama hicho wanataka mchakato usitishwe, wengine wanataka
uendelee,” alisema.
Mbatia
alisema Ukawa inashangazwa na Rais Kikwete kwa kitendo chake cha
kufanya ziara ya kutembelea ranchi binafsi ya kufugia wanyama ya
aliyekuwa Rais wa Marekani, George Bush wakati nchi ikiwa katika
sintofahamu ya mchakato wa kupata Katiba Mpya huku watu wa kada
mbalimbali wakitaka mchakato usitishwe.
Profesa
Lipumba alisema: “Wapo wanaosema kuwa Ukawa tumegawanyika. Hilo siyo
kweli kwa sababu waliotusaliti na kuhudhuria vikao vya Bunge hata
asilimia tano hawafiki. Zaidi ya asilimia 95 hatujakwenda bungeni,”
alisema.
Alisema
kuwa Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph
Warioba alitenga masuala ya ardhi, maliasili na Serikali za Mitaa ili
yaingizwe katika Katiba ya Tanganyika, hivyo kuyajadili mambo hayo
katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano si sahihi. Mbowe alisema: “Viongozi
wanaiacha nchi ijiendeshe yenyewe. Ni kama ndege ambayo rubani yupo
lakini ameweka ‘auto pilot’, yaani wameiruhusu ndege ijiendeshe
yenyewe.”
CAG achunguze
Kuhusu
suala la ukaguzi wa hesabu, Mbatia alisema katika vikao vya Bunge la
Bajeti, baadhi ya wabunge walihoji zinakopatikana fedha za kuendesha
Bunge la Katiba na kusema kutokana na hali hiyo, ni vyema CAG
akachunguza kwa undani suala hilo.
Hoja
kutaka Bunge hilo lisitishwe inaungwa mkono na makundi mbalimbali
pamoja na baadhi ya wabunge wa CCM, akiwamo Naibu Katibu Mkuu wa CCM,
Mwigulu Nchemba (Iramba-Magharibi) aliyesema likiendelea bila uhakika wa
kupata akidi ya uamuzi itakuwa ni kupoteza zaidi ya Sh20 bilioni za
walipa kodi na wananchi hawataelewa.
Hata
hivyo, uongozi wa Bunge umesisitiza kuwa vikao hivyo ambavyo awali
vilifanyika kwa siku 67, vitaendelea kwa siku 60 za kazi zilizoongezwa
na Rais Jakaya Kikwete, bila kuhusisha siku za Jumamosi na Jumapili
ambazo zinaongeza muda wa wajumbe kukaa Dodoma kuwa 84.
Post a Comment