PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: UKAWA WAENDELEA KUITESA SERIKALI WAAPA KUTOKURUDI BUNGE MAALUM LA KATIBA...Cheki hii
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Freeman Mbowe  akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa ha...


Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Freeman Mbowe  akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.  Wanaomfuatia ni wenyeviti wenza wa umoja huo James Mbatia (katikati) na Profesa Ibrahimu Lipumba. Picha na Edwin Mjwahuzi  
“Wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisema kuwa suala la muundo wa serikali lilitakiwa kupigiwa kura, Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samwel Sitta anaendelea kuongoza Bunge kama mchakato ni mali yake binafsi. Baadhi ya viongozi wa chama hicho wanataka mchakato usitishwe, wengine wanataka uendelee,” alisema.
Mbatia alisema Ukawa inashangazwa na   Rais     Kikwete kwa kitendo chake cha kufanya ziara ya kutembelea ranchi binafsi ya kufugia wanyama ya aliyekuwa Rais wa Marekani, George Bush wakati nchi ikiwa katika sintofahamu ya mchakato wa kupata Katiba Mpya huku watu wa kada mbalimbali wakitaka mchakato usitishwe.
Profesa Lipumba alisema: “Wapo wanaosema kuwa Ukawa tumegawanyika. Hilo siyo kweli kwa sababu waliotusaliti na kuhudhuria vikao vya Bunge hata asilimia tano hawafiki. Zaidi ya asilimia 95 hatujakwenda bungeni,” alisema.
Alisema kuwa Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba alitenga masuala ya ardhi, maliasili na Serikali za Mitaa ili yaingizwe katika Katiba ya Tanganyika, hivyo kuyajadili mambo hayo katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano si sahihi. Mbowe alisema: “Viongozi wanaiacha nchi ijiendeshe yenyewe. Ni kama ndege ambayo rubani yupo lakini ameweka ‘auto pilot’, yaani wameiruhusu ndege ijiendeshe yenyewe.”
CAG achunguze
Kuhusu suala la ukaguzi wa hesabu, Mbatia alisema katika vikao vya Bunge la Bajeti, baadhi ya wabunge walihoji zinakopatikana fedha za kuendesha Bunge la Katiba na kusema kutokana na hali hiyo, ni vyema CAG akachunguza kwa undani suala hilo.
Hoja kutaka Bunge hilo lisitishwe inaungwa mkono na makundi mbalimbali pamoja na baadhi ya wabunge wa CCM, akiwamo Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba (Iramba-Magharibi) aliyesema likiendelea bila uhakika wa kupata akidi ya uamuzi itakuwa ni kupoteza zaidi ya Sh20 bilioni za walipa kodi na wananchi hawataelewa.
Hata hivyo, uongozi wa Bunge umesisitiza kuwa vikao hivyo ambavyo awali vilifanyika kwa siku 67, vitaendelea kwa siku 60 za kazi zilizoongezwa na Rais Jakaya Kikwete, bila kuhusisha siku za Jumamosi na Jumapili ambazo zinaongeza muda wa wajumbe kukaa Dodoma kuwa 84.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top