Hatimae ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zanzibar
uliokua umekwama kwa muda mrefu, umeanza kwa kasi huku ujenzi huo ukitarajiwa
kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kisauni nje
kidogo ya mji mkuu wa nchi ya Zanzibar, Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano, Dk. Juma Malik Akil, alisema hitilafu zilizotokea hapo awali
tayari zimeshafanyiwa kazi na ujenzi unaendelea .
Alisema mradi huo uliosita miaka miwili iliyopita kwa sababu
mbali mbali unaendelea tena chini ya kampuni ya Kichina ya BCEG ikisimamiwa na
Mshauri Elekezi Kampuni ya ADPI kutoka Ufaransa.
Alisema juhudi za serikali katika kuwaletea maendeleo
wananchi wake ikiwa na pamoja na kuwajengea miundombinu muhimu ambayo itakuwa
chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa nchi ya Zanzibar
itaendelea.
Alisema lengo la serikali kujenga uwanja huo ni kufikia
hadhi ya kimataifa ambayo itaweza kuitangaza nchi ya
Zanzibar na kuongeza idadi ya watalii.
Uwanja huo hadi kumalizika kwake utagharimu dola za Marekani
milioni128 ambazo ni mkopo wakutoka benki ya Exim ya China na unategemewa
kuchukuwa abiria milioni 1.6 kwa mwaka na kutua ndege kubwa ikiwemo Airbus A340
na Boeing 777.
Mratibu wa mradi huo,Yassir Dicosta, aliwaomba Wazanzibari
kutoa hofu kuhusu jengo hilo.
Mshauri elekezi kutoka kampuni ya ADPI ya Ufaransa, Jean
Mare, alisema kazi yake kubwa ni kuangalia ujenzi huo unavyokwenda.
Post a Comment