PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: HALI INATISHA???: WANASWA WAKISAFIRISHA WATOTO 13 KWENDA NCHINI KENYA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
              JESHI la polisi mkoani Tanga,limenasa mtandao haramu wa usafirishaji na  kufanikiwa kuwakomboa watoto 1...




             
JESHI la polisi mkoani Tanga,limenasa mtandao haramu wa usafirishaji na  kufanikiwa kuwakomboa watoto 13,waliokuwa wakisafirishwa kuelekea nchi jirani ya Kenya.

Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga,SACP Frasser Kashai ametoa taarifa za tukio hilo jana akisema kuwa watuhumiwa wa usafirishaji wa watoto hao wanashikiliwa na polisi kwa hatua zaidi za kisheria na mahojiano.


Kamanda Kashai alisema kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 12,mwaka huu saa 17.30 jioni huko wilayani Mkinga mkoani hapo eneo la Horohoro mpakani na nchi jirani ya Kenya.

Kashai aliwataja watoto waliookolewa ni Zalika Abeid (16)Bisura Husein (16)Mwanaid Husein (18) wote wa kijiji cha Ntamwe wilayani Lushoto na Asimaya Sekanyorota (20)Ashiruna Sekanyorota (20) ambao ni familia moja wa Wanga Lushoto na  Seleman Ibrahim (20) wa Maligwe Lushoto.

Wengine ni Rajabu Mohamed(15) wa Kwamnele Handeni,Mgaza Twaha (15) wa Mtamwe Lushoto,Mussa Ayubu (17) wa Mlole Lushoto Abdully Hassani (17) mkazi wa Mlole wilayani Lushoto mkoani hapo.

Pia wamo Ally Adam (16) wa Kwamnele Handeni,Said Husein (22)wa kijiji cha Wangwe Lushoto na Idd Rajabu wa mkazi wa Baga wilayani Lushoto.

Kwa mujibu wa kamanda Kashai ni kwamba wanaoshikiliwa na polisi ni dereva wa gari lililokuwa likisafirisha watoto hao SaLUM Hassan(39) na Hassan Salim (39) mkazi wa Lushoto aliyekuwa muangalizi wa watoto hao na kwamba sasa unafanyika utaratibu wa kuwapata wazazi wa watoto ili kurejeshwa makwao.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa watoto hao walikuwa wakipelekwa kwenye chuo cha kiislamu kiitwacho Ummukuluthummu Muslim School huko Mombasa ambapo hata hivyo taratibu za kisheria kwa usafiri wan je ya nchi hazikufuatwa.

Kamanda Kashai aliongeza kwa kusema kwamba watoto hao walikuwa wakisafirishwa kwa gari lenye nambari T702 CRZ Toyota Hiace huku ukaguzi ulipofanyika kwenye hati za kusafiria iligundulika kuwa haukutiamia kutokana na kukosekana kwa barua za ridhaa kutoka kwa wazazi wao.

Kutokana na tukio hilo kamanda Kashai amewataka wananchi kufuata taratibu za kisheria kwa kuwasiliana na idara ya Uhamiaji pindi wanapotaka kusafiri kwenda nje ya nchi ambayo itasaidia kuepuka uwezekano wa kujitokeza kwa vitendo vilivyo kinyume na taratibu za kisheria kwa kuzingatia misingi ya haki.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top