Kutoka kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta (TPB), Sabasaba
Moshingi, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka na baadhi ya
viongozi meza kuu wakiwa wameshikana mikono na kuinyanyua juu ikiwa ni
ishara ya kuwaunganisha wastaafu kwenye fursa mara baada ya uzinduzi wa
mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF
leo jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi akizungumza
katika hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu
wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka (wa nne kulia), Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi (wa tano kulia)
wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki
katika mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni
wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa TPB na LAPF wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa mpango
maalumu ulioandaliwa na Benki ya Posta (TPB) wa kutoa mikopo kwa
wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa mfuko wa Pensheni LAPF, wakipitia kwa umakini kipeperushi
cha TPB kilicho na maelezo juu ya mpango wa Mikopo kwa Wastaafu.
Mstaafu
ambaye ni mwanachama wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Mzee Gondwe
akielezea namna alivyopata mkopo kupitia TPB na kumpa matumaini ya
maisha mapya baada ya kustaafu.
Post a Comment