Moja ya jengo la Shule ya Sekondari Erikisongo iliyopo Wilayani Monduli mkoani Arushaa likiwa linawaka moto |
ZAIDI ya wanafunzi 100 wa Shule ya Sekondari Erikisongo iliyopo Wilayani Monduli mkoani Arusha, wamenusurika kifo baada ya vyumba vitano vya mabweni yanayotumiwa na Wavulana kuteketea kwa moto mapema leo asubuhi.
Aidha, mashuhuda wamesema kuwa tukio hilo limetokea leo Julai 23, 2014 majira ya saa nne asubuhi na kuwa chanzo cha moto huo kinatajwa kuwa ni hitilafu ya umeme iliyotokea wakati wanafunzi wote wakiwa darasani, na kuwa hakuna mtu yoyote aliyedhurika licha ya mali kadhaa za wanafunzi zimeteketea. Mmoja wa mshuhuda hao, Josam Amani, amesema Jeshi la Polisi, Kitengo cha Zima mkoani humo, walifika katika eneo la tukio wakati mabweni hayo yakiwa yamekwisha kuteketea kwa moto.
Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa, ametembelea Shule hiyo na kuahidi kugharamikia kuwasafirisha wanafunzi majumbani kwao, wakati utaratibu unafanywa kurejesha katika hali ya kawaida. Mapema mwaka jana Serikali ilitoa kauli ya kuzitaka shule zote za bweni kuhakikisha kuwa zinakata bima ya moto kwa lengo la kuchukua tahadhari ya majanga ya moto sambamba na kuwa na uhakika wa kupata fidia ya mali.
Aidha, kumbukumbu zinaonyesha kuwa baada ya majanga hayo kutokea wanafunzi wanalazimika kutumia baadhi ya vyumba vya madarasa kwa malazi, jambo ambalo linatajwa kuweza kuathiri maendeleo ya kitaaluma kwa wanafunzi shuleni kutokana na baadhi ya wanafunzi kuwa katika kipindi cha maandalizi ya mtihani mablimbali ikiwemo mitihani ya Taifa.
Wakati huo huo Gari lateketea kwa moto mitaa ya Mbauda – Arusha Taarifa zilizotufikia punde kutoka mkoani humo zinadai kuwa gari la kubebea mizigo aina ya Fuso lisilotambulika namba zake mara moja, limeteketea kwa moto jioni ya jana saa 6:45, katika barabara ya Arusha Dodoma.
Post a Comment