Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam,Suleiman Kova akizungumza na
Vyombo vya habari mbalimbali mapema leo makao makuu ya jeshi la polisi
jijini Dar kuhusiana na sakata la viungo vya binadamu vilivyokamatwa
jana ambapo Kamanda Kova amesema kuwa watu wanane wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo.
Kamanda
Kova amesema kuwa jopo la Wataalamu saba limeundwa kuchunguza tukio
hilo na amethibitisha kuwa viungo vile vilikuwa ni vya maiti,ambavyo
hutumika na madaktari kwa elimu ya matibabu na utafiti.
UKWELI KUHUSU VIUNGO VYA BINADAMU VILIVYOKAMATWA BUNJU,
Habari
zimethibitisha kwamba masalia ya viungo vya binadamu vilivyotupwa
maeneo ya Bunju yametoka chuo cha udaktari IMTU kilichopo Mbezi baada ya
wanafunzi kumaliza kutumia kwa mazoezi. Viungo hivi vilitupwa baada ya
mukosa pesa za kuteketeza kwenye tanuri maalum.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.