Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI)Isaya Mngulu akishauriana na maafisa wake leo |
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI)Isaya Mngulu |
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai nchini (DCI),
Issaya Mungulu, katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Arusha jana, Jumanne Julai 22, 2014 imedaiwa kuwa Julai 21, 2014 saa 2.00
usiku katika maeneo ya Sombetini, Jeshi hilo limewakamata Yusufu Ally
(30) na mkewe Sumaiya Juma (19) wakiwa nyumbani kwao baada ya kupekuliwa
walikutwa na mabomu ya kutupwa kwa mkono Saba (7), risasi sita za
bunduki aina ya shortgun, mapanga mawili, unga wa baruti unaokadiriwa
kufika nusu kilo na bisibisi moja.
Mungulu amesema kuwa Yusufu ni miongoni mwa
watuhumiwa waliokuwa wanatafutwa kwa ulipuaji wa mabomu maeneo yote
jijini Arusha na kuwa mahojiano juu ya mtuhumiwa bado yanaendelea dhidi
yake.
Aidha, amesema uchunguzi wa shauri hilo pamoja na matukio mengine ya
milipuko yanaendelea ikiwa ni pamoja na kuwahoji watuhumiwa walioko
mikononi mwa polisi na kuwakamata watakaobainika kuhusika na matukio
hayo.
Mtuhumiwa mwingine wa milipuko nchini asakwa na Polisi
Hata hivyo, Jeshi hilo limesema linamtafuta, Yahya Hella (33) mkazi wa
Mianzini mkoani humo, mwenyeji wa Chemchemu, Kondoa – Dodoma kwa tuhuma
za kuhusika na matukio ya ulipuaji mabomu nchini.
Watuhumiwa wengine kufikishwa mahakamani
Amesema kufuatia tukio la mlipuko wa bomu Julai 7, 2014 saa 22.15 usiku
katika mgahawa wa VAMA, eneo la gymkhana Jijini Arusha, ambapo watu
wanane walijeruhiwa vibaya, Jeshi hilo limewakamata watuhumiwa 25 kwa
uchunguzi na kuwa kati yao watu sita watafikishwa Mahakamani mapema
iwezakanavyo.
Amewataja watuhumiwa watakaofikishwa Mahakamani kwa tukio hilo kuwa ni
pamoja na Shaaban Mmasa (26) ambaye ni mlinzi aliyekuwa zamu siku hiyo
kwenye mgahawa huo, Athuman Mmasa (38) na Mohamed Nuru (30), wote
walinzi katika Mgahawa wa Chinese uliopo eneo la Gymkhana jirani na eneo
la tukio.
Wengine ni Sheikh Jaffar Lema (38) ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi
Olturmet katika wilaya ya Arumeru, pia alikuwa Imam wa Msikiti wa QUBA
mjini Arusha ambaye ametambuliwa kama mmoja wa viongozi walioratibu
matukio ya milipuko ya mabomu maeneo balimbali nchini, Abdul Salim (31),
wakala wa Mabasi Stendi Arusha, na Said Temba; umri wa miaka 42,
mfanyabiashara wa Arusha. .
Post a Comment