Title: Veta Tanzania na Kenya wasaini ushirikiano
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5
Des:
Arusha, Chuo cha Elimu ya Ufundi Stadi(VETA) Jijini Arusha pamoja na Chuo cha Utalii cha Kenya ( KUC) wamesaini makataba wa makubalia...
Arusha, Chuo cha Elimu ya Ufundi Stadi(VETA) Jijini Arusha pamoja na Chuo
cha Utalii cha Kenya ( KUC) wamesaini makataba wa makubaliano kwa ajili
ya kuboresha mafunzo ya sekta ya hoteli na utalii .
Wakuu wa vyuo hivyo, Mkuu wa Veta
Tanzania, Mhandisi Zebadiah Moshi na Mkuu wa Chuo cha Veta Kenya, Dk ,
Kenneth Ombongi walisaini makubaliano hayo juzi.
Mhandisi Moshi alisema wakuu wa vyuo hivyo wamekubaliana kuendesha
mafunzo katika sekta ya hoteli na utalii kwa walimu ili waweze
kufundisha vizuri wanafunzi wanaochukua masomo hayo.
Alisema soko la huduma za hoteli na utalii linakuwa kwa kasi kubwa
hali inayopelekea ukosefu wa wahudumu wenye utaalam wa hali ya juu wa
kuhudumia hoteli za kitalii na kupelekea aira kuwa za wageni pekee.
"makubaliano hayo yatasaidia kupata uzoefu wa kubuni mbinu mpya
za kupata wanafunzi bora wenye utaalam wa juu na wa kati katika
kuhudumia hoteli na sekta ya utalii ambayo inakuwa kwa kasi"alisema
Naye Mkuu wa Chuo kutoka Kenya (KUC) Dk, Ombongi alisema Kenya
imejipanga katika kuhakikisha sekta ya utalii na hoteli inakuwa kwa
kasi na walianza kutoa huduma hiyo muda mrefu zaidi ndio maana hivi
sasa wanashirikiana na Veta Tanzania ili kuweza kupata soko zuri kwa
nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika sekta ya utalii na hoteli.
Wakati huo huo, Mkuu wa Chuo hicho, Flora Hakika alisisitiza kuwa chuo
hicho kimejipanga katika kuhakikisha kinatoa wanafunzi bora katika
sekta ya utalii na hoteli wataaoweza kupata ajira kwani serikali
imejenga chuo hicho kisasa zaidi ili kusaidia walimu kutoa mafunzo kwa
kiwango cha juu na kuzalisha ajira kwa wanafunzi wanaomaliza chuoni
hapo.
Post a Comment