“Ni wito wetu kwa wadau wa uchaguzi nchini kuwa elimu ya uraia na elimu ya mpiga kura, lazima ianze kutolewa angalau mwaka mmoja kabla ya uchaguzi na sio kufanyika ndani ya miezi sita kabla ya siku ya kupiga kura,” alisema Kibamba.
Pia aliitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), vyombo vya usalama na vyombo vya habari kusimamia majukumu yao kikamilifu ili kulinda usalama wa raia, mali zao na Taifa.
Alisema NEC inatakiwa kurekebisha daftari la wapiga kura angalau mara mbili ndani ya miaka mitano ili kuwapa haki ya msingi wananchi ambao wanakosa haki hiyo.
Pia alishauri kuwa siku ya kupiga kura Tanzania ifanywe kuwa siku ya katikati ya wiki na kutangazwa kuwa ni siku ya mapumziko ili kuruhusu watu wa kada mbalimbali kupata fursa ya kupiga kura na kuongeza kuwa mchakato wa Katiba unaoendelea ukamilike ipasavyo ili kuandaa vyombo vikuu vya uwajibikaji vya kikatiba.
Post a Comment