Uongozi
wa klabu ya Young Africans unapenda kuwajulisha wanachama wake, wapenzi
wa soka na wadau kwa ujumla kuwa taarifa za kuhama kwa wachezai wake
Didier Kavumbagu na Frank Domayo kwenda kujiunga na Azam FC
zisiwakatishe tamaa, ni mapenzi ya wachezaj wenyewe kwani
walishakubaliana na uongozi kila kitu juu ya kuendelea kuitumikia Yanga
kabla ya siku mbili hizi kuonekana wakiwa wamejiunga na wana ramba
ramba. Yanga tayari ina wachezaji watatu wenye
mikataba inayoendelea na kama kanuni za VPL kwa wachezai wa kimataifa
kuwa watatu zitatumika wachezaji Haruna Niyonzima, Hamisi Kizza na
Emmanuel Okwi ndio watakaoendelea, hivyo uongozi uliomba mwongozo kwa
TFF juu ya taratibu zitakazotumika kwa msimu ujao kabla ya kuwasainisha
Kavumbagu na Twite.
Awali uongozi wa Yanga ulikuwa kwenye
mazungumzo na wachezaji hao tangu mwanzoni mwa msimu wa 2013/2014 juu ya
kuongezewa muda wa mikataba yao ili waweze kuendelea kuitumika Yanga
kwa ajili msimu mpya ujao 2014/2015.
Didier Kavumbagu na Mbuyu
Twite ambao mikataba yao ilikuwa mwishoni waliongea na uongozi tangu
mapema mwaka jana mwezi wa Septemba juu ya kuweka sahihi zao na
kuendelea kuitumikia Yanga na kukubaliana mambo yote ya msingi kikubwa
kilichokuwa kinasubiriwa ni maamuzi ya TFF juu ya usajili wa wachezaji
wa kigeni msimu mpya wa 2014/2015 kwani Azimio la Bagamoyo linapaswa
kuanza kutekelezwa msimu huu
Uongozi wa Yanga uliandikia TFF
barua mapema kuomba kupewa mwongozo wa kanuni zitakazotumika kwenye
usajli kwa wachezaji wa kimataifa kwa msimu mpya kufuatia Azimio la
Bagamoyo kuelekeza msimu huu kila timu inapasa kuwa na wachezaji watatu
wa kigeni, mpaka sasa uongozi wa Yanga haujapata majibu juu ya utaratibu
utakaotumika kwenye msimu wa Ligi Kuu ijayo.
Hivyo makubaliano
ya wachezaji Didier Kavumbagu, Mbuyu Twite na uongozi wa Yanga SC
yalikua yakisubira majibu ya TFF juu ya kanuni zipi zitakazotumika
kwenye usajili msimu wa 2014/2015 kwa wachezaji wa kigeni na katika hali
ya kushangaza Kavumbagu akaonekana tayari ameshasaini kuichezea timu ya
Azam FC.
Kuhusu Frank Domayo aliyeripotiwa jana kujiunga na
Azam FC pia alikuwa katika makubaliano ya kuongeza mkataa tangu mwezi
Julai 2013, alikubaliana na uongozi juu ya mambo yote ya msingi na
kilichobakia ilikuwa ni kuweka sahihi kwenye mkataba mpya, lakini Domayo
alisema hawezi kusaini mpaka siku atakapokuja mjomba wake ambaye ndie
wakala wake na ahadi hiyo iliendelea kwa muda wa mwaka mzima kabla ya
jana kusikia ameshasaini timu nyngine.
Habari hizi zimewashitua
wapenzi, wanachama na washabiki wa Young Africans lakini ukweli ni kuwa
wachezaji wenyewe walishindwa kuwa wakweli kwa viongozi na mwisho wa
siku walikua na mipango yao ya kuondoka, hivyo uongozi ulijtahid kadri
ya uwezo wake lakini wachezaji wanaonekana hawakua tayari kuendelea
kuichezea Yanga SC.
Taarifa kamili kuhusu mipango ya timu kwa
msimu ujao pamoja na ripoti ya kocha mkuu Hans pamoja na benchi lake la
Ufundi zitatolewa hivi karibuni baada ya benchi la ufundi na uongozi
kukaa kwa pamoja na kuafikiana mipango ya msimu ujao.
Aidha
uongozi wa Yanga SC unawaomba wanachama wake, wapenzi na washabiki
wasiwe na wasi wasi juu ya kuondoka kwa wachezaji hao kwani Yanga bado
ina nafasi wachezaji wengi wenye vipaji na itaendelea kuboresha kikosi
chake kwa kuzingatia maelekezo ya kocha mkuu Hans katika usajli wa msimu
ujao
About Author
Journalist , Enterpreneur, Lecturer and Blogger. Email :ngoboleaa@gmail.com.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment