Habari
zilizotufikia mtandao huu hivi punde zinasema kuwa
serikali ya mkoa wa Shinyanga imesitisha huduma ya fast Track katika
hospitali ya mkoa wa Shinyanga ambako hivi karibuni huduma za matibabu
katika hospitali hiyo zimepanda mfano katika kupanda huko kwa huduma za
matibabu akina mama walikuwa wanalazimika kujifungua kwa gharama ya
shilingi elfu 70,na kama ni ulikuwa unahitaji kupasua jipu basi
ingekulazimu kulipia huduma hiyo shilingi elfu 40,kumwona daktari
shilingi 10,000?= na mengine mengi. Akitoa ufafanuzi kuhusu hoja ya mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga kupitia ccm Azza Hilal kwenye mkutano wa wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Shinyanga,aliyetaka kujua imekuwaje gharama za matibabu zikapanda katika hospitali ya mkoa bila kufuata utaratibu unaotakiwa tena limepitishwa bila kupata baraka za kikao cha baraza la ushauri la mkoa. Mbunge huyo na wajumbe wengine wa mkutano huo wamedai kuwa kitendo cha bodi ya afya ya mkoa kupitisha suala la kupanda kwa gharama za matibabu katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga huenda ni njama za wapinzani kukidhoofisha chama cha mapinduzi hasa katika kipindi hiki ambako chama kinaelekea katika uchaguzi na kuongeza kuwa kitendo cha kupandisha gharama za matibabu ni kukifanya chama kichukiwe na wananchi. Kufuatia hoja ya mbunge huyo wa viti maalum na wajumbe wengine walioonesha hali ya kutoridhishwa na kupanda kwa gharama za matibabu wakati wananchi wengi maisha yao ni duni,mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga amesema serikali kuanzia sasa imesitisha huduma hiyo kwa ajili ya maslahi ya wananchi na chama tawala kwani kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu kupanda kwa gharama za matibabu kupanda katika hospitali hiyo wakati wananchi wengi ni maskini. "Bodi ya afya imekosea,sasa tunasitisha kwa muda,hata mimi nilishtushwa na taarifa za kupanda kwa gharama za matibabu,huu utaratibu nausitisha,kesho nitatoa barua/waraka maalum kuhusu suala hili,kweli linaumiza wananchi wetu,nitakaa na bodi hii tuangalie namna ya kushughulika na jambo hili",ameeleza Rufunga. Haya yamejiri wakati huu katika mkutano wa wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Shinyanga unaoendelea hivi sasa katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga ambao umehudhuriwa na watendaji wakuu wa serikali,wakuu wa wilaya,wakurugenzi wa halmshauri,wenyeviti wa halmashauri za wilaya,mkuu wa mkoa,katibu tawala wa mkoa n.k. |
About Author
Journalist , Enterpreneur, Lecturer and Blogger. Email :ngoboleaa@gmail.com.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment