PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MAUAJI YA KUTISHA YATOKEA HUKO MKOANI NJOMBE
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Hali Ya Matukio ya Mauaji Imeanza Kuongezeka Katika Maeneo Mbalimbali Mkoani Njombe Huku Sababu Kubwa Ikitajwa Kuwa ni Imani za Ki...
Hali Ya Matukio ya Mauaji Imeanza Kuongezeka Katika Maeneo Mbalimbali Mkoani Njombe Huku Sababu Kubwa Ikitajwa Kuwa ni Imani za Kishirikina.

Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limethibitisha Kutokea Kwa Matukio Mawili Tofauti ya Mauwaji Huku Likimtafuta Neema Mwalongo Kwa Tuhuma za Kuhusika na Kifo cha William Kibiti Miaka 40.

Kwa Mujibu wa Taarifa ya Jeshi la Polisi Iliyotolewa Kwa Vyombo Vya Habari na Kusainiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani Inaelezeza Kuwa  Marehemu William Kibiti Alifariki Akiwa Anapatiwa Matibabu Katika Kituo cha Afya cha Makambako Baada ya Kupigwa na Mti wa Mwanzi Sehemu za Kichwani .

Taarifa Hiyo Imeeleza Kuwa Tukio Hilo Limetokea Wakiwa Kwenye Kilabu cha Pombe za Kienyeji Majira ya Saa Mbili Usiku Katika Kijiji cha Utengule.

Aidha Taarifa Hiyo Pia Imesema Tukio la Pili Limetokea Kijiji cha Ibiruko Wilayani Makete Ambapo Rafiki Kibiniwasi
Ngala Miaka 75 Alikutwa Ameuwawa Ndani ya Nyumba Yake Kwa Kukatwa na Kitu Chenye Ncha Kali Sehemu za Paji la Uso Wake .

Mwili wa Marehemu Rafiki Kibiniwasi Ngala Uligunduliwa Mei 19 Mwaka Huu Majira ya Saa Mbili Usiku na Beny Kibinuwasi Kamge,.
 
Matukio Yote Yametokea Kati ya Mei 18 na 19 Mwaka Huu Huku Jeshi Hilo Likiendelea Kuwatafuta Watuhumiwa wa Matukio Hayo Pamoja na Kufanya Uchunguzi wa Kina Kuhusiana na Matukio.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top