PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: TAARIFA RASMI KWA UMMA YA KIFO CHA MKUU WA WILAYA YA KALAMBO MHE. MOSHI CHANG'A, KUZIKWA JUMATANO MKOANI IRINGA.
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA MKOA WA RUKWA Anuani ya simu:”R...


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MKOA WA RUKWA
Anuani ya simu:”REGCOM” Simu Na:(025)-2802138/2802144
Fax Na. (025) 2802217
Baruapepe: rasrukwa@yahoo.com


OFISI YA MKUU WA MKOA,
S.L.P. 128,
SUMBAWANGA.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella M. Manyanya (Mb) kwa masikitiko makubwa anapenda kuwajulisha juu msiba mkubwa ulioukumba Mkoa wetu wa Rukwa wa kuondokewa na Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mhe. Moshi Mussa Chang’a (62) aliyefariki jana jioni terehe 20 April, 2014 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Shinikizo la Damu na Kisukari.
Mwili wa Marehemu Mhe. Chang’a unategemewa kusafirishwa kesho jioni kutoka Jijini Dar es Saam hadi nyumbani kwao Mkoani Iringa ambapo mazishi yake yatafanyika keshokutwa siku ya Jumatano tarehe 23 April, 2014.
Marehemu Mhe. Chang’a alizaliwa Mkoani Iringa Januari Mwaka 1952 na amewahi kushika nafasi mbalimbali Serikalini na katika Chama cha Mapinduzi (CCM). Katika nafasi ya Ukuu wa Wilaya amewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Mbeya, Tabora, Mkalama na Kalambo Mkoani Rukwa ambapo mauti yake yamemfika.
Katika Ngazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) amewahi kuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Njombe na Iringa Vijijini na Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Iringa.
Marehemu Mhe. Chang’a ameacha watoto watano (5) na Mjukuu Mmoja (1).Watoto wa kiume 3 na Wakike 2.
Kwa niaba ya Wananchi wa Mkoa wa Rukwa tunatoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki, na wote walioguswa na msiba huu mkubwa. Tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Sisi tulimpenda lakini Mungu kampenda zaidi.
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema peponi “AAAMIN”
Imetolewa na:
OFISI YA MKUU WA MKOA
RUKWA
Tarehe 21 April, 2014.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top