PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: SOMA HAPA KAULI YA MBOWE DHIDI YA UKAWA KUTOKA BUNGENI JANA!!!!!!!!!!!
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Leo katika kipindi cha KUMEPAMBAZUKA kinachorushwa hewani na kituo cha Radio cha RADIO ONE STERIO nimemsikia Kamanda A...
 
















Leo katika kipindi cha KUMEPAMBAZUKA kinachorushwa hewani na kituo cha Radio cha RADIO ONE STERIO nimemsikia Kamanda Aikael Freeman Mbowe akitoa ufafanuzi wa UKAWA kutoka nje ya bunge maalumu la katiba na kutorudi tena bungeni bali kwenda kwa wananchi.Mheshimiwa Mbowe ameeleza jinsi ambavyo bunge linavyoendeshwa kwa upendeleo mkubwa sana,Matusi makubwa ya nguoni kwa wajumbe wenye mawazo tofauti na ya serikali ya ccm,kutumia vitisho vingi,udhalilishaji na uonevu mkubwa .

Mheshimiwa Mbowe ametolea mfano kwamba Kama Lukuvi amekwenda kanisani na kuanza kuhutubia watu kwamba kama serikali 3 zitapita Jeshi litachukua nchi.Hivi ni vitisho ambavyo kwanza vinampunguzia umakini ama uwezo rais aliyepo madarakani na pia ni kuamsha hisia za jeshi kufanya hivyo hata leo.Kwa maneno mengine ni kuwapa mawazo ama maoni wanajeshi wetu kupindua serikali.

Inashangaza sana Mheshimiwa Lukuvi hawezi kuwajibika kwa kauli hii kwani mwaka 2009 Samson Mwigamba aliwahi kuandika makala fulani kwenye gazeti la TANZANIA DAIMA kuhusu jeshi lakini serikali ya ccm ikamfungulia mashtaka mahakamani kwamba ni mchochezi na analitaka jeshi LIASI TAIFA NA KUFANYA MAPINDUZI ( ARMY MULTINY AND REVOLUTION) na bahati nzuri sana kesi ile Mwigamba alishinda mwezi Fenruary 2014.Je serikali haioni kwamba Lukuvi ameamsha hisia na kufanya uchochezi jeshi kuasi????

Hata hivyo,mimi binafsi nadhani ccm wanakiinimacho wananchi.Wananchi wamesema Wanataka serikali 3 wao wanatoa vitosho vya Muungano kuvunjika,wanatoa vitisho kwamba nchi itaingia vitani,wanatoa vitisho kwamba fanya ufanyalo ni serikali 2 tu na mwingine akasema kwamba hata kama wananchi wanataka serikali 3 basi wasubiri yeye aondoke madarakani kwanza.

HIVI statements kama hizo zinaashiria dalili za nia njema kweli( GOOD POLITICAL WILL) ya kupata katiba mpya kweli???.Nina mashaka makubwa sana kama kweli katiba mpya inaweza kupatikana katika hali hii ?
http://themonthlyjob.com/?refcode=8192

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top