PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: RAIA WA GHANA AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA PITIA HAPA KKUPATA UNDANI WA HABARI HII
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Wiki iliyopita, mtu mmoja mwenye uraia wa Ghana kwa jina Boubacar Traore (42), alikamatwa na kilo 3.5 za heroin zenye dhamani ya dola za ...
http://gopaidweekly.com/?ref=80557

Wiki iliyopita, mtu mmoja mwenye uraia wa Ghana kwa jina Boubacar Traore (42), alikamatwa na kilo 3.5 za heroin zenye dhamani ya dola za Kimarekani milioni 3 mara tuu baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JFK, jijini New York, Marekani.
Aliwasili uwajani hapo kwa ndege ya British Airways ikitokea London alikounganisha ndege.

Taarifa zilizowasilishwa mahakamani zinaonyesha kuwa Traone alianzia safari yake Tanzania lakini haijaelezwa alipitia JNIA au KIA. Hata hivyo, jana Rais Kikwete alisema kuwa kuwa dawa za kulevya zinazidi kupita katika viwanja vya ndege vya JNIA na KIA na kuwa hali hii inazidi kuchafua heshima na jina la Tanzania.

Maafisa uwanjani hapo (JFK) walishtukia begi moja (Samsonite roller bag) ambalo lilikuwa limekaa kama halina mwenyewe vile. Baada ya kulichunguza walikuta kuwa mmiliki wake alikuwa ni Traone ambaye ni baba wa watoto saba anayemiliki grocery nchini Ghana. Baada ya begi hilo kupekuliwa maafisa hao walikuta kilo 3.5 za heroin zilizokuwa zimefichwa kwenye begi hilo kama linavyoonekana kwenye picha hapo chini.



Baada ya kukamatwa Traore alikiri kosa lake la kushiriki katika kujaribu kuingiza dawa hizo za kulevya Marekani na kukubali kushirikiana na polisi ili kumkamata mshiriki mwingine. Baada ya kupiga simu kadhaa, Traore alikubaliana kwenye simu kukutana na mtu mwingine kwa jina Francis Abankwa (50) ambaye ni devera wa moja ya mabasi ya MTA (Metropolitan Transportation Authority).

Abankwa alikuwa amepanga kuchukua mzigo mida ya saa kumi jioni lakini alimwambia Traore asubiri kidogo mpaka round ya mwisho kwa sababu basi lilikuwa limejaa abiria wengi. Hivyo, walikubaliana kukutana saa 6.51 za jioni kwa saa za New York katika kituo cha basi cha Grand Concourse and East Tremont kilichopo Bronx, jijini New York. Wakati huo, Abankwa alikuwa bado hajui kuwa Traore alikuwa tayari ameshakamatwa na dawa hizo. Pia hakujua kuwa alikuwa amekubali kushirikiana na Homeland Security kumkamata na yeye pia.

Baada ya Abankwa kuwasili katika kituo cha basi cha Grand Concourse and East Tremon na basi lake, Traone alipanda kwenye basi hilo akiwa na begi lililokuwa na dawa hizo za kulevya. Baada ya kupanda basi, Abankwa aliendesha basi lake huku wakijadiliana juu ya dili lao la dawa za kulevya. Mazungumzo yao yote yalikuwa yanarekodiwa na kifaa ambacho Traore alivalishwa na polisi.



Pia kwenye basi hilo kulikuwa na maafisa wawili waliokuwa wamevaa nguo za kiraia na walipanda basi mapema kabisa kutokea huko lilipoanzia na kujifanya kama abiria wa kawaida. Maafisa hao walishuka kituo cha pili kabla y kufikia kituo cha mwisho. Baada ya basi kufika kituo cha mwisho, abiria wote waliobakia walishuka ispokuwa Traore aliyebakia kwenye basi na kurudi na dereva Abankwa hadi kwenye depot ya mabasi ya MTA (Kingsbridge Depot) iliyopo Inwood.



Baada ya kuliacha basi pale, walielekelea kwenye gari ya Abankwa na ndipo polisi wapowazunguka na kumkamata Abankwa ambaye wakati huo alikuwa na lile begi mikononi mwake. Abankwa ambaye yupo katika kituo cha mahabusu cha Metropolitan kilichopo Brooklyn amefikishwa mahakami na kushtakiwa. Traore nae ameshtakiwa lakini kwa mujibu wa rekodi za kimahakama amepewa dhamana kwa bond ya dola 100,000.

Abankwa amefanya kazi MTA miaka nane na mwaka 2012 alilipwa dola za Kimarekani 102,000 kama mshahara pamoja na marupurupu mengine. Mwezi February mwaka huu alishtakiwa kwa fraud baada ya kuchukua Medicaid benefits kwa ajili ya mke na mtoto wake.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top