Wananchi
wa mji wa Dodoma wakiangalia sehemu ya madhara ya tukio la moto
uliotokea usiku wa kuamkia leo katika baadhi ya maduka yaliopo kwenye
Barabara ya Nyerere Karibu na Makao makuu ya CCM mjini Dodoma,moto huo
umeteketeza maduka matatu na mgahawa wa New Chick Villa Reustaurant. Maduka
yaliyoathirika na moto huo ni Gulio La Mahafa Duka lililokuwa linauza
bidhaa mbali mbali kwa jumla na reja reja zikiwamo bidhaa za
Bakhresa,Duka la Esheki Investment lililo kuwa likiuza bidhaa za
maofisini,vitabu na huduma ya uchapaji pomoja na Duka la madawa la
lijulikanalo kama Kavula Pharmacy.
Kila aliekatiza katika eneo hilo akusita kusimama na kuangaria athari hiyo ya moto kwenye Maduka hayo.
Sehemu
iliyokuwa na maduka ikiwa imeteketea kabisa kwa moto uliotokea leo
Barabara ya Nyerere karibu na Ofisi za makao makuu ya Chama cha
Mapinduzi CCM.
Post a Comment