PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MNYIKA ASIKITISHWA NA MAJIBU YA MKUU WA MKOA WA DAR KUHUSU BODABODA NA BAJAJI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), ameeleza kutoridhishwa na majibu yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq, ku...


MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), ameeleza kutoridhishwa na majibu yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq, kuhusu mgogoro unaoendelea juu ya usafiri wa pikipiki ‘bodaboda’ na bajaj

Mnyika alisema jana kuwa mkuu huyo wa mkoa alitoa kauli hiyo kutokana na kumuandikia ujumbe, akimtaka asitishe kwa muda utekelezaji wa tamko lake, ili kupisha mazungumzo kati ya serikali, wahusika wa bodaboda, bajaj na wadau wengine.“Nimepitia sheria inayohusika ambayo ni The Surface and Marine Transport Regulatory Authority Act, Sheria namba 9 ya mwaka 2001, hakuna kifungu chochote kinachokataza pikipiki au bodaboda na bajaj kuingia katika maeneo ya katikati ya jiji, hivyo mkuu wa mkoa anapaswa kutoa ufafanuzi kwa umma ni sheria ipi anaitumia,” alisema Mnyika katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana.Alisema Sadiq anapaswa kuzingatia kwamba sheria hiyo kifungu cha 5 imetamka kwamba wajibu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) ni kulinda maslahi ya watumiaji wa huduma na kuhamasisha upatikanaji wa huduma, ikiwemo kwa wateja wa kipato cha chini.“Usafiri wa pikipiki/bodaboda na bajaj sio tu umetoa fursa ya ajira kwa vijana, bali pia unasaidia wananchi wa kipato cha chini na pia unasaidia katika mazingira ya foleni katika Jiji la Dar es Salaam, hivyo agizo la kutaka usafiri huo uishie Buguruni, Ubungo, Tazara na Chuo cha Uhasibu ni suala ambalo limeibua mgogoro unaostahili ufumbuzi wa haraka,” alisema Mnyika.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top