Madiwani Kiteto kwenda kumwona Pinda ili awatatulie mgogoro wa ardhi
mwenyekiti wa HALMASHAURI YA KITETO
Ni Kuhusu kujitokeza mauaji ya wakulima na wafugaji
Wasema vigogo wapo nyuma ya migogoro hiyo
NA. MOHAMED HAMAD 0758 222248 BARAZA la madiwani wa Halamshauri ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyaralimeunda tume maalumu ya kwenda kumwona Waziri Mkuu Mizengo Pinda ilikutatua migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji inayoendeleakurindima kila kukicha
Akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani jana (juzi) Mussa Britoni Diwani wa (CCM) kata ya Sunya alisema kutokana na kukiukwa kwamaagizo ya Waziri Pinda juu ya kushughulikia migogoro hiyo wameamuakurejea kwake kueleza ukweli wa mambo
"Waziri Pinda aliagiza kufanyika vikao vya vijiji saba vilivyounda hifadhi hiyo ambapo alisema anatilia shaka hifadhi hiyo akisema kamakuna hifadhi mbona alichokiona ni mashamba ya wakulima? wananchiwaulizwe kwanza kama nia yao bado ya kuendelea na hifadhi hiyo"alisemaPinda kwenye mkutano wa hadhara Wilayani humo
Pinda alisema kwa kuwa kuna utata wa mipaka uliowekwa na Halamshauri kinyemela katika eneo hilo la Hifadhi ya Emboley Murtangos Wilayaiweke utaratibu upya na shirikishi ambao utasaidia kubainisha mipakahiyo kuondoa tatizo hilo
Kutobainishwa kwa mipaka hiyo kumeibua migogoro ya mara kwa mara wa ardhi ambapo hadi hivi sasa kila mara maafa yanazidi kujitokeza katiya wakulima na wafugaji kwa kuingiliana kishuhuli kilimo na ufugaji
Waziri Pinda alitoa agizo hilo Jan 16 mwaka huu kutaka Halmashauri hiyo kubainisha mipaka kazi ambayo hadi hii leo haijafanyika nakusababisha makundi hayo kutojua mipaka wako wako katika eneo ganikati ya kilimo,mifugo, makazi ama hifadhi
Wakati Serikali ikitoa agizo la kutolewa elimu kwa pande hizo SerikaliWilayani Kiteto imeendelea kuwakamata wakulima na wafugaji nakuwafikisha kwenye vyombo vya sheria mahakamani kasha kufungwa kifungocha mwaka mmoja jela ambapo zaidi ya watu 50 walifungwa huku 12wakiachiwa huru baada ya kukutwa ndani ya eneo hilo
Post a Comment