JESHI la Polisi nchini, limeshindwa kuwafikisha mahakamani
watuhumiwa wa madawa ya kulevya katika mkoa wa Manyara, ambapo kwa
sasa Polisi wamekamata misokoto ya bangi 2676 na mirungi bunda 70
katika mkoa huo, huku likishindwa kakabiliana na hali hiyo kutokana na
Askari wake kushiriki vitendo hivyo katika maeneo mbalimbali hapa
nchini.
Aidha kumbukumbu zinaonyesha kuwa katika kipindi cha Machi, mwaka
2012, Jeshi hilo mkoani Kilimanjaro lilimshikilia Askari wake (G 842,
Konstebo Deogratius), ambaye alikamatwa na misokoto mine ya bangi
akiwa katika ukumbi wa disko wa Albeto uliopo mjijni Moshi, huku
akifanya vurugu katika ukumbi huo ambapo pamoja na Jeshi la Polisi
mkoani humo kuthibitisha tukio hilo, mtuhumiwa huyo akisukwa rumande
pamoja na Askari mwingine ambaye aliingia katika ukumbi huo akiwa na
bunduki aina ya SMG na kufanyia watu fujo.
Mbali na matukio hayo Jeshi hilo, lilitoa taarifa ya kukamata kwa
watuhumiwa 45 wakihusishwa na matukio ya utumiaji wa bangi, mirungi na
gongo katika msako wa kuimarisha doria katika maeneo mbalimbali mkoani
humo, msako ambao hadi leo Polisi mkoani humo wameshindwa kuwafikisha
makahamani watuhumiwa wakidai bado uchunguzi haujakamilika.
Misokoto 2676 ya bangi yakamatwa
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Deusdedit Nsimeki, amemwambia Mwandishi
wetu kuwa Aprili 15 saa 11:30 asubuhi katika eneo la Minjingu barabara
ya Arusha-Babati, walimkamata, Nassoro Idd (27) mburege mkazi wa
Singida mjini akiwa na misikoto ya bangi 2000 akiwa anatumia usafiriwa
basi la kampuni ya Mtei lenye namba T.449 CAL, lililokuwa likitokea
Arusha kwenda Singida.
Amesema siku hiyo hiyo huko minjingu Kata ya Nkaiti, Askari waliokuwa
doria walimkamata, Juma Khatibu (18) Mshilazi na mkulima wa Arusha,
akiwa na bangi misokatomo 620, iliyokuwa imehifadhiwa ndani ya mikate
iliyokuwa imetobolewa, ambapo mtuhumiwa alikuwa ni abiria wa basi la
kampuni ya Kandahar lenye namba T. 391 BUR lililokuwa likitokea Moshi
kwenda mkoani Singida.
Aidha Nsimeki, alisema katika Kata ya Nkaiti, wilayani Babati, Riziki
Ferisi (18) Mchaga na mkulima wa moshi alikutwa na bangi misokoto 56
akiwa kwenye basi la Mtei lenye namba T.991 ABC, lililokuwa likitokea
Moshi kwenda Singida, ambapo Aprili 13 maeneo ya magugu, Edward Mollel
(27), Janeth Mollel (27 na Mudi Robert (33) kwa pamoja walikuwa
wanasafirisha madawa ya kulevya aina ya Mirungi bunda 70 yaliyokuwa
kwenye gari aina ya Noah yenye namba T.339 BYE, inayomilikiwa na
Edward Mollel, mkazi wa Singida.
“Pamoja na kuwa kuna mbinu mpya zinatumika kusafirisha madawa haya,
ikiwemo kuweka kwenye siti za magari kama Noah,’Tyubu’ za matairi ya
magari, mifuko mbalimbali na mabegi, na kuweka ndani ya mikate
iliyotobolewa lakini bado tumegundua mbinu hizo” alisema Nsimeki.
Amesema kuwa, Jeshi hilo limejizatiti kwa kuhakikisha kuwa
hakuna makosa ya uhalifu, yatakayovunja amani katika maeneo yote ya
mkoa huo katika kipindi hiki cha sikukuu za Pasaka.
Walimiki wa mabasi kukumbana na mkono wa sheria
Sanjari na watuhumiwa hao kukamatwa,Jeshi hilo limesema litachukuahatua kwa wamiliki wa mabasi, ambayo yatapatikana na madawa hayoyakiwemo yaliyokamatwa katika zoezi hilo, huku akitoa wito kwawananchi wa mkoa huo kutoa ushirikiano wa dhati kwa Jeshi hilo, ilikuwabaini watuhumiwa mablimbali
Home
»
»Unlabelled
» JESHI LA POLISI MKOANI MANYARA LATUHUMIWA KUTOWAFIKISHA WATUHUMIWA WA MADAWA YA KULEVYA MAHAKAMANI
About Author
Journalist , Enterpreneur, Lecturer and Blogger. Email :ngoboleaa@gmail.com.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment