IRINGA: WAKULIMA WA NYANYA IRINGA WATAKIWA KUUNDA VIKUNDI A+ A- Print Email PRINCE MEDIA TZ Link Author Title: IRINGA: WAKULIMA WA NYANYA IRINGA WATAKIWA KUUNDA VIKUNDI Author: PRINCE MEDIA TZ Rating 5 of 5 Des: Wakulima wa nyanya mkoani Iringa, wameshauriwa kujiunga katika vikundi ili waweze kunufaika na mi... Wakulima wa nyanya mkoani Iringa, wameshauriwa kujiunga katika vikundi ili waweze kunufaika na misaada mbalimbali pamoja na mikopo kutoka katika taasisi za fedha ikiwamo benki na vicoba ili kuinua thamani ya mazao wanayozalisha. Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Gelard Guninita wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wakulima wa Nyanya iliyofanyika katika Kijiji cha Nzih Tarafa ya Kalenga mkoani hapa. Maadhimisho hayo yaliandaliwa na Muunganisho wa Ujasilimali Vijijini (Muvi) kwa ushirikiano na wadau wa kilimo kutoka sekta binafsi. Kwa mujibu wa taarifa za taasisi hiyo, zao la nyanya katika mkoa huo limeongezeka kutoka tani 100,009 mwaka 2010 na kufikia tani 100,400 kwa kipindi cha mwaka 2013 katika maeneo ambayo taasisi hiyo imekuwa ikifanya kazi. Akizungumza katika maadhimisho hayo, Guninita, ambaye alikuwa akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma alisema ikiwa wakulima hao wataunda vikundi na kusajili, watakuwa wametambuliwa na kuwa na sifa za kupata mikopo katika taasisi za fedha jambo linaloweza kuwasaidia kupata mitaji kwa ajili ya kuendesha shughuli zao. “Ninaomba mjiunge katika vikundi na sisi serikalini tunasaidia pale itakapoonekana kuna ulazima,” alisema.
Post a Comment