NA. MOHAMED HAMAD
WANANCHI Wilayani Kiteo Mkoani Manyara wamemtaka Mkurugenzi Mtendaji
wa Halamshari hiyo Bw. Ndunguru aliyeshika nafasi ya Bi Jane Mutagurwa
aliyehama kuondoa ukabila uliopo
Wakizungumza hayo wamesema ukabila huo unasababishwa na baadhi ya
Viongozi wa Siasa na Serikali kwa maslahi yao binafsi na kwamba
wamemtaka Mkurugenzi kuondoa ukabila
Bakari Maunganya ambaye ni mkulima Wilayani hapo amesema mbali na suala la
ukabila rushwa imetawala kwenye vyombo vya sheria hali inayowanyima
haki wananchi wanapohitaji haki
Akizungumza na wadau wa maendeleo mara baada ya kuwasili Wilayani humo
Ndunguru aliwataka watumishi wa Halmashauri kuwa na utamaduni wa
kupendana na kuacha majungu
Wilaya ya Kiteto inakabiliwa na matatizo lukuki yakiwemo migogoro ya
ardhi,huduma duni za afya, elimu, pamoja na ubovu wa miundombinu
ambayo unasababishwa na usimamizi mbovu wa miradi hiyo
MKURUGENZI WA KITETO ATAKIWA KUONDOA UKABILA!!!!!!
Title: MKURUGENZI WA KITETO ATAKIWA KUONDOA UKABILA!!!!!!
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
NA. MOHAMED HAMAD WANANCHI Wilayani Kiteo Mkoani Manyara wamemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halamshari hiyo Bw. Ndunguru aliyeshika nafasi...
Post a Comment