Baraza Kuu la Waislamu nchini Kenya SUPKEM na Baraza la
Ushauri kwa Waislamu KEMNAC yamelaani vikali shambulio na mauaji ya
jana katika kanisa la Joy Jesus huko Likoni Mombasa.
Viongozi wa mabaraza hayo wamelaani shambulio hilo lililopelekea watu wanne kuuawa na kuwataka Wakenya kuweka kando itikadi zao za kidini na badala yake kuviunga mkono vyombo vya usalama vya nchi hiyo katika vita dhidi ya ugaidi.
Aidha viongozi wa Kikristo nao wametoa taarifa ya kulaani shambulio hilo la kigaidi ambapo watu wawili wenye silaha walivamia kanisa la Joy Jesus huko Likoni Mombasa na kuwamiminia risasi waumini waliokuwa kanisani hapo.
Samuel Kimohu mmoja wa wachungaji waandamizi katika kanisa hilo, ameitaka serikali ya Rais Uhuru Kenyatta kuchukua hatua za haraka na kuwashughulikia waliotekeleza shambulio hilo.
Wakati huo huo, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Kenya amesema kuwa, vikosi vya usalama vimeimarisha ulinzi ili kukabiliana na hatua yoyote ile ya kigaidi. Inspekta Jenerali David Kimaiyo amesema kwamba, tayari kikosi chake kimeanza uchunguzi kuhusiana na shambulio hilo la jana la kigaidi mjini Mombasa.

Post a Comment