Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limetangaza
kuwa, litachukua hatua za kuhakikisha kwamba, linazuia kutokea maafa ya
chakula katika Jamhuri ya Afrika ya Kati kutokana na mauaji
yanayoendelea kufanywa na kundi la Kikristo la Anti-Balaka dhidi ya
Waislamu.
Shirika hilo limeatangaza kuwa, linapanga kuanzisha mpango wa ustawi wa kilimo, kudhamini chakula kinachofaa kwa wote, kupambana na lishe duni na kuboresha chakula cha watu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na maeneo mengine duniani.
Tayari FAO imetiliana saini na serikali ya muda ya Bangui, mpango wenye thamani ya dola milioni nane. Wakati huo huo, mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali yameendelea kutahadharisha kuhusiana na hali mbaya ya kibinadamu inayowakabili wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati hususan Waislamu. Mamia ya Waislamu wameuawa na maelfu ya wengine kujeruhiwa katika mashambulizi yanayoendelea kufanywa na wanamgambo wa Kikristo wa Anti Balaka katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Post a Comment