Kikundi cha Kimataifa cha Mawasiliano kimeandaa kongamano kubwa
la kuchunguza njia za kulikwamua taifa la Madagascar kutoka katika
mgogoro wa baada ya uchaguzi mkuu nchini humo. Kongamano hilo
litakalofanyika siku ya Ijumaa ijayo mjini Antananarivo, litakuwa na
jukumu la kuchunguza uongozi wa Rais Hery Rajaonarimampianina tangu
kiongozi huyo alipochukua madarakani ya nchi.
Kundi hilo linaundwa na wawakilishi kutoka taasisi mbalimbali ukiwemo Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya, Jumuiya ya Ustawi ya Kusini mwa Afrika SADC, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Kamisheni ya Bahari ya Hindi (COI), Jumuiya ya Kimataifa ya Nchi Zinazozungumza Kifaransa (OIF) na Soko la Pamoja la Kusini na Mashariki mwa Afrika (COMESA).
Afisa mmoja wa Umoja wa Afrika nchini Madagascar amesema kuwa, kikao hicho ambacho kitajadili njia za kurejesha utawala wa katiba baada ya kumalizika uchaguzi mkuu nchini humo ni cha pili baada ya kile cha kundi hilo kilichomalizika huko mjini Addis Ababa Ethiopia. Rais Rajaonarimampianina alishinda kwa asilimia 53,49 katika uchaguzi uliofanyika tarehe 20 mwezi Disemba mwaka jana.

Post a Comment