PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: CRIMEA YAONGEZA MSUGUANO KATI YA RUSSIA NA EU
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Crimea yazidisha uadui kati ya Russia,  Wamagharibi Suala la kujitenga eneo la Crimea kutoka Ukraine na kujiunga na Russia limeendelea ...




Crimea yazidisha uadui kati ya Russia,
 Wamagharibi Suala la kujitenga eneo la Crimea kutoka Ukraine na kujiunga na Russia limeendelea kuzidisha uadui kati ya Moscow na nchi za Magharibi.Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, William Hague, amesema kuwa London na waitifaki wake wa Ulaya wanapanga kuiweka vikwazo vya muda mrefu serikali ya Russia ambayo ameituhumu kuwa inatishia usalama na amani barani Ulaya. Hague amesema Russia itaondolewa kwenye Jumuiya za kimataifa ili kupunguza ushawishi wake. Pia amesema ushirikiano wa kijeshi kati ya Russia na nchi za Ulaya utapunguzwa.Waziri huyo wa Uingereza pia amezitaka nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kupunguza kiwango cha gesi kutoka Russia na kutafuta vyanzo mbadala vya nishati kutoka kwa mataifa mengine. Siku chache zilizopita, Marekani ilipitisha vikwazo dhidi ya mashiriki kadhaa ya Russia pamoja na watu binafsi wanaoaminika kuwa karibu na Rais Vladmir Putin. Moscow nayo ilijibu mapigo kwa kutangaza vikwazo dhidi ya mashirika kadhaa ya Marekani pamoja na wafanyabiashara binafsi na wanasiasa mashuhuri wa nchi hiyo akiwemo Spika wa Kongresi pamoja na Maseneta kadhaa.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top