PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Mamlaka ya mji mdogo Karatu yang'owa vibarua wazembe
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  NA SOPHIA FUNDI KARATU. maipacarusha20@gmail.com Baraza la mamlaka ya mji mdogo halmashauri wilaya ya KARATU mkoani Arusha  imeazimia kwa ...

 





NA SOPHIA FUNDI KARATU.


maipacarusha20@gmail.com

Baraza la mamlaka ya mji mdogo halmashauri wilaya ya KARATU mkoani Arusha  imeazimia kwa pamoja kuwaondoa vibarua wote wanaopoteza mapato ya mamlaka hiyo.


Kauli hiyo imetolewa Leo na wenyeviti wa mamlaka ya mji mdogo wa KARATU katika kikao Chao Cha kawaida kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri.


Akizungumza na wenyeviti hao mwenyekiti wa mamlaka hiyo Yuda Morrata alimwagiza Afisa mtendaji wa mamlaka wakishirikiana na idara ya Fedha kuwaondoa vibarua wote wanaopoteza mapato ya Mamlaka kwa njia zozote zile kwani wanawakwamisha katika kufikia malengo waliyojiwekea  ya ukusanyaji wa mapato ya Mamlaka.


"Mweka hazina tunakuagiza kawatoe vibarua wote wanaopoteza mapato ya Mamlaka hasa eneo la kituo Cha mabasi ndio hasa wanaopoteza mapato kwa kuleta mkanganyiko katika ukusanyaji"alisema Morrata


Amesema kuwa wamejiwekea mkakati kwa kuunda kikosi kazi itakayoingia mtaani  kwa ajili ya kukusanya mapato kwani Hadi sasa wako nyumba sana kwa ukusanyaji wa mapato ambapo wamekusanya asilimia 61 tu mpaka mwezi huu Jambo  ambalo amesema  ni kushindwa kufikia malengo ya asilimia 80au 100.


Aliwataka wenyeviti  kutoa ushirikiana kwa kikosi hicho  kwa kuwaonyesha  maeneo yote yatakayofikiwa ili kuhakikisha wanafikia malengo.


Akizungumza na wenyeviti hao katibu wa Ccm Shabani Mrisho amesema kuwa chama hicho kimeandaa mafunzo maalum kwa ajili ya baadhi wataalam wa halmashauri na wenyeviti wa mamlaka ili kuondoa mwingiliano wa kazi baina yao.


Amesema kuwa kumekuwa na migogoro ya mara kwa mara na baina ya pande hizo aidha kea kutojua mipaka yao ya kazi au kutojua kazi zao hivyo mafunzo hayo yatakuwa suluhisho la migogoro hiyo yatakayofanyika hivi karibuni.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top