Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya A.Mashariki James Millya Akizungumza kwenye kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa vyombo vya habari Duniani, kwa Mkoa wa Arusha Jijini humo. |
Waajiri wa kampuni za habari nchini, wametakiwa kuzingatia kanuni za ajira kwa kuwalipa waandishi iliowaajiri malimbikizo ya madeni yao ya mishahara kwa kuwa na wao wanastaili kupata ujira huo ili waweze kujiendesha kimaisha.
Wito huo umetolewa Jana na Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Tanzania, James Millya aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa vyombo vya habari Duniani kwa Mkoa wa Arusha.
Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa vyombo vya habari Duniani huazimishwa Mei3 ya kila mwaka na mwaka huu kwa Tanzania kitaifa yalifanyika visiwani Zanzibar ambapo Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi alikuwa mgeni rasmi.
Millya alisema kumekuwepo na malalamiko ya muda mrefu ya waandishi wa habari juu ya kutolipwa mishahara yao na baadhi ya kampuni wanazozifanyia kazi jambo ambalo ni uvunjifu wa haki za binaadam na haliwezi kukubalika mahala popote.
" Mimi ni mwanasheria kitaaluma na ni mtetezi wa haki za binaadam, nilisomea sheria kuja kutetea jamii ya wanyonge na wote hapa mnanifahamu, suala la maslahi ya waandishi ni haki za binaadam, waandishi mnastahili kulipwa vizuri ili muendeshe maisha yenu, kama Kuna mwajiri awalipi waandishi anafanya makosa makubwa," amesema.
Amesema kauli mbiu ya maadhimisho hayo inayosema " kuunda mustakabali wa haki, uhuru wa kujieleza kama kichocheo Cha haki nyingine zote za binaadam" ni vyema waajiri wa vyombo vya habari pia wakazingatia kauli hiyo na kulipa waandishi madai yao lakini pia kuboresha maslahi zaidi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya Klabu ya waandishi wa habari Arusha, Claud Gwandu amesema waajiri wamekuwa wakitumia waandishi wa habari kama sehemu ya wao kujitengenezea kipato kutokana na kutokuwepo kwa sheria rafiki zinazowabana ili waweze kulipa maslahi Bora kwa waandishi.
Hata hivyo ameipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa madai kuwa ameonyesha nia ya kuboresha maslahi ya waandishi wa habari na hivyo ana imani sheria ambazo zimekuwa kikwazo kwa waandishi wa habari zinaenda kufanyiwa maboresho kama alivyoahidi.
Mwenyekiti wa JOWUTA Mussa Juma akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari Mkoa wa Arusha. |
Akitoa mada kuhusu changamoto za waandishi wa habari Nchini na umuhimu wa kujiunga na Chama vya wafanyakazi, Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyakazi waandishi wa Habari Nchini (JOWUTA), Mussa Juma amesema baadhi ya waandishi wamekuwa wakifariki kutokana na msongo wa mawazo unaotokana na kutolipwa maslahi yao kwa muda mrefu.
" Kuna baadhi ya waandishi wa habari wamefariki kutokana na msongo wa mawazo, unakuta mtu anasomesha, familia inaumwa, bado familia inahitaji kula unaenda kumdai mwajiri pesa zako anakwambia hana, hili ni tatizo kubwa sana ambalo sisi kama Jowuta tumeliona na tunaanza kulifanyiakazi hivi karibuni,"amesema.
Mwenyekiti wa APC Claud Gwandu |
Mussa amesema Jowuta inajipanga na hivi karibuni itaanza kuwafikisha mahakamani baadhi ya waajiri ambao wameshindwa kuwalipa Wafanyakazi wao mishahara kwa muda mrefu na kuitaja Moja ya kampuni kuwa ni Sahara Media ambayo wanyakazi wake wanadai zaidi ya bilioni1 za malimbikizo ya mishahara na fedha za hifadhi ya jamii.
Katika kongamano hilo ambapo wageni mbalimbali walihudhuria ikiwemo uongozi Chama Cha Waandishi wa Habari wanaojitegemea nchini Kenya ambao walitoa uzoefu wao juu ya tasnia ya habari.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na makundi ya waandishi wa habari Mkoa wa Arusha na wageni waalikwa |
Post a Comment