PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: HIVI KWELI TATIZO NI UWEPO WA SIMBA NA YANGA,AU UZITO WA UDUMAVU WA FIKRA ZETU?
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Na: Erick D. Nampesya Nianze kwa kusisitiza kwa Mimi Erick David Nampesya,ni Shabiki wa Simba Sports Club tangu mwaka 1974,hadi siku nitak...


 


Na: Erick D. Nampesya


Nianze kwa kusisitiza kwa Mimi Erick David Nampesya,ni Shabiki wa Simba Sports Club tangu mwaka 1974,hadi siku nitakaporejea kwa Baba Muumba,na katika Vitu ninavyojivunia na Kufurahia ni Pamoja na Kushabikia Mnyama.

Zamani simba ikifungwa nilikuwa napata Taabu sana ila bahati nzuri nikaja kuwa Mwandishi wa Habari/Mtangazaji hali iliyoniweka karibu zaidi na Michezo mingine lakini zaidi Soka kwani Hakuna Ubishi kwamba ndio unaaongoza kwa kupendwa na Walio wengi Duniani,na kwa wengi imekuwa Fursa kubwa kimaisha kuanzia Wachezaji,Viongozi,Makocha,Madaktari ma Wataalam mbali mbali,na karibia kila mdau anapata anachostahili.Namshukuru Mungu kwa sasa hata ikifungwa siumiikama miaka ya Ujanani kwenye miaka 18-35 hivi.


Nikirejea kwenye Kichwa cha Habari hapo juu,Niseme tu kwamba katika mambo yaliyonipa Taabu hasa wakati huo nikiwa Mtangazaji Redioni,ni Upinzani toka kwa Mashabiki na wakati Mwingine Matusi pale inapotokea Umeripoti au Kuandika Habari ambacho Shabiki wa Simba au Yanga hakijamvutia kwa sababu zake,na kwa Makusudi kabisa nilijikuta nikikabiliana na Maneno machafu kutoka kwa Watu ambao kwa Heshima zao sikuwatarajia kama wanaweza kuwa na Ufinyu wa fikra kiasi hicho.


Mfano mmoja Hai,siku moja nikiwa Ofisini Dar es Salaam,Yanga Ilitwaa Ubingwa wa Soka Tanzania Bara,baada ya kushinda Mechi moka jioni hiyo na hivyo kufikisha Alama ambazo zisingeweza kufikiwa na Timu nyingine katika zilizokuwa zinawania Ubingwa.

Kwangu mimi kimaadili na Utendaji wetu ilikuwa ni Habari kubwa jioni hiyo na ambayo tunakuwa wa Kwanza kwenda nayo Hewani yaani Breaking News,hivyo nikapiga Simu Studio London wakajiunga nami nikatangaza Habari hiyo jioni hiyo hiyo.

Kwangu mimi kama ni Pongezi pengine ningepewa na Producer au Boss wangu kazini kwa Kuwapa Story mpya ambayo vyombo vingine vitairipoti baadae usiku au kwenye Magazeti ya kesho yake,lakini Cha Ajabu Rafiki zangu mashabiki wa Yanga wakaanza Kunipa Pongezi ambazo sikuona unuhimu wake kwani ilikuwa ni sehemu yankazi yangu

,Huku Mashabiki wa simba wakinibatiza Umamluki kwamba tulijua wewe Mwenzetu ni simba kumbe Yanga mkubwa,mmoja nilimjibu Je,nikiwa Shabiki wa simba ulitaka niseme Yanga imetwaa Ubingwa Batili na kwa hiyo simba ndio mabingwa ili ufurahi wewe,kisha nikaongezea Neno wewe na Wapumbavu wenzako mlitaka Niseme Simba ndio Bingwa ili mfurahi???.

Siku nyingine Simba ikaja Mwanza kucheza dhidi ya Toto Africa,Ikawa inacheza Mpira wa kiwango cha chini mno,huku kwenye bench hata Maji ya kunywa wakilazimika kukimbilia maduka ya pembeni ya uwanja na kuja Kuwapa wachezaji,Wakati wa Mapumziko BBC wakajiunga nami Live kuwapa kinachoendelea CCM Kirumba,Wakati huo Simba ikiwa nyuma bao 2-1,nikasema kwa Mpira unaochezwa na Simba,Itakuwa Vigumu kuamini kuwa Simba hii ndiyo msimu uliopita iliivua ubingwa wa Africa Zamalek,nikaongeza kuwa haitashangaza Ikifungwa hata bao 4,utadhani Toto walinisikia kwani Matokeo ya Mwisho Toto 4 Simba 2 (sina hakika sana ila Simba alipewa 4)Niliporejea Studio Nikatangaza kile kile kilichotokea.

Siku hiyo kama si Msaada wa Maaskari rafiki zangu pale uwanjani nadhani ingekuwa Balaa kubwa,maana mashabiki wa simba walinizonga baada ya mechi wakinituhumu kwamba mimi ni Pandikizi ndani ya Simba ili ni shabiki wa Yanga,sikuhitaji kuwabembeleza ila niliwaambia Hebu kama mnaweza badilisheni Matokeo kisha Mtangaze mtakavyoona inawafaa.

Ninayo mifano mingi mno ya moja kwa moja kwangu lakini mingine nasoma magazetini,Yaani kwa shabiki wa simba ili muelewane unapaswa kutangaza mabaya ya Yanga kuanzia Januari mosi hadi December 31,kadhalika wa Yanga naye lazima utangaze Mabaya simba kwa siku 365 ikibidi kwa saa24,hapo mtaelewana,Vinginevyo haufai hata robo.

Tatizo jingine ni Upotoshaji makusudi unaofanywa na wale ambao wameaminiwa na chombo anachofanyia kazi ili mradi tu afurahishe upande mwingine yaani Simba au Yanga yaani utadhani Uhai wetu na Hatima ya Maisha yetu,umeshikiliwa na Timu hizo,ambalo kwangu mimi linanishangaza sana.

Kuna Rafiki yangu mkubwa sana Anaitwa Yahya ni shabiki wa Yanga,binafsi ananikubali kwamba hana shaka na Utangazaji wangu Redioni na ananiheshimu na kunikubali mno,ila akaongeza kuwa Ushikaji wetu uishie hapo hapo usivuke,ikitokea Yanga wameanzisha Redio kisha akasikia kwa mfano Nimepata kazi kwenye Redio hiyo inayomilikiwa na Yanga huku yeye akiwa masomoni Nchini Marekani,atakuwa radhi kujilipia ticket ya kuja Tanzania kuhakikisha tu ninapoteza  kibarua changu,kisha anarudi zake Masomoni US kwa sababu tu Erick ni shabiki wa Simba,basi tukacheka sana na Urafiki wetu unaendelea kama kawaida.Huyo hatanii kabisa na niseme kabisa ni mmoja wa marafiki zangu na ndio msimamo wake na tunaheshimiana kwenye hilo.

Wapo mashabiki wa Simba,wenye kustaarabika na hata Yanga pia ila naamini wanazidi kupungua pande zote kutokana upinzani wa hawa wasioelewa ambao mimi nawaita wakati mwingine wamejaaliwa kipaji cha Upumbavu.

Utagundua hayo Pale inapotokea Mwamuzi akavurunda  mfano Mechi ya Simba na Azam leo ikaonekana mnufaika wa makosa hayo ni Simba basi ataitwa ni shabiki wa Simba,na mwamuzi huyo akikosea mechi ya Yanga vs Mtibwa akinufaika,Yanga wale mashabiki watamhamishia Yanga.

Mashabiki hawakubali kwamba hapa Nchini tuna tatizo la Waamuzi bali wanajua kuwa Waamuzi ni Mashabiki wa simba na Yanga wala siyo kwamba uelewa na weledi wao wa sheria ndilo tatizo la msingi ambalo kama nchi linapaswa kutafutiwa Ufumbuzi.


Imefikia sehemu uadilifu wa Mtu hata kwenye kazi ya Kitaaluma,unapimwa tu kwa ushabiki wa simba au Yanga,hata watangazaji wenzangu wengi wameamua kuficha mapenzi yao kwa Simba au Yanga,kwa kwa hofu mashabiki wenye kipaji cha upumbavu.

Mwamuzi akiongeza muda wa mchezo kwa mujibu wa sheria ataitwa wa timu fulani,yaani imekuwa taabu tu.

Hivi sasa Nchi imetawaliwa na Mjadala  wa Kama Simba iliwahi kufika Nusu fainali kombe la Shirikisho wale wa Yanga wanadai Timu yao ndiyo ya Kwanza kutoka Tanzania kufika hatua hiyo,Naomba niwaulize, miaka ile Ligi kuu ikiitwa Ligi daraja la kwanza Bingwa wa wakati ule rekodi yake tuifute tu,kwa sababu hivi sasa inaitwa Ligi kuu??Rekodi za Liverpool kutwaa Ubingwa wa England kabla ya mfumo wa sasa,Nani kasema zilifutwa?Sasa Naomba Wasiojua simba Ilifika nusu fainali Klabu Bingwa Afrika na si lazima ukubali maana kukataa pia ni haki yako ya msingi na ya Kikatiba ila haitabadilisha Ukweli huo maana Ukweli una Tabia ya kusafiri katika Mstari mnyoofu kama Mwanga.


Mchambuzi Jemedari Jemedari Said Kazumari ,hivi sasa anashambuliwa kila kona eti yeye ni shabiki wa Simba,kwa sababu tu,anapenda kufafanua ukweli bila kujiumauma,Sasa Najiuliza Mashabiki mnataka kwa wiki Watangazaji waweke Ratiba kuwafurahisha mashabiki wa simba sikui 3na nusu na Yanga siku 3 na nusu?Watangazaji hawawezi kuwa Wapumbavu kiasi hicho.

Moja ya mambo ninayoyachukia ni unafiki Na inakuwa mbaya zaidi pale hata viongozi wa juu Kitaifa wanapoamua kuwa Wanafiki eti wasionekane ni Wanashabiki Timu gani kati ya hizo Maarufu tofauti na Ukubwa unaolazimishwa na mashabiki hao,Mbona Rais wa Zanzibar anaweka wazi kuwa Yeye ni shabiki wa Yanga,tatizo liko wapi?Mbona mheshimiwa JK hafichi kuwa yeye ni Shabiki na Mwanachama wa Yanga na amewahi kushiriki Michezo michafu kuisaidia Yanga,kosa liko wapi?

Binafsi napenda kila Mtu afanye kazi yake Mtangazaji au mchambuzi akifanya kazi yake tusiache ya msingi wa hoja na kukimbilia kutafuta anashabikia timu gani,kwa sababu hakuna kipengele kinachomzuwia kupenda timu yoyote.


Chini chini Leodgar Tenga anasifiwa pengine na mashabiki wa Simba kwa sababu pamoja na kuchezea Yanga lakini kwenye Uongozi wa TFF,hakuleta Ubabaishaji mfano lile suala la Yanga kugoma kuingiza kagame cup vs simba,mwaka 2008 kama sikose,na si ajabu Yanga wakawa hawakufurahia uongozi wake kwa sababu hizo hizo.

Naye Jamal Malinzi si ajabu anapendwa na kukumbukwa na Mashabiki wa Yanga shauri ya Ubabaishaji aliofanya kuiumiza simba.


Ni kutokana na hali hii ambapo hata viongozi wakubwa wakiwemo mawaziri,Wabunge linapokuja suala la yanga au simba wataongea maneno hadi unajiuliza maswali magumu mno kichwani,Je tatizo ni Uwepo wa simba na Yanga au Mashabiki wamekubali kudunisha Fikra zao kila leo?

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top