Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi |
Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi baada ya kwasoma US Monastir katika mechi zao mbili akizishuhudia kwa macho yake kisha kuangalia mechi za mikanda ya video amefunguka kuwa wanakazi ya kuwachunga mastaa wanne wa timu hiyo watakaovaana nao Jumapili hii mjini Tunis.
Amefichua kwamba wapishi wa US Monastir ni mabeki wao wawili wa pembeni. Amewataja wengine kuwa ni kiungo wao wa kati na nahodha wao huku pia wakiwa na mshambuliaji anayejua kufunga kwa vichwa katika safu yao uya ushambuliaji.
.
“Tunatakiwa kuwa makini na hao wachezaji wanne, timu yao inategemea ubora wao katika kutengeneza mashambulizi lakini mtu wa kumalizia ni huyo mshambuliaji wao, tutatafuta akili ya jinsi ya kuwadhibiti.”
Post a Comment