Mtangazaji wa TBC Grace Henry Kingalame aliyeteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Nyang’halwe mkoani Geita |
NA: ANDREA NGOBOLE, PMT
Jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia
Suluhu Hassan alitangaza uteuzi wa wakuu
wa wilaya wapya 37, kuwahamisha vituo vya kazi wakuu wa wilaya 48 na wengine 55
kubakia katika vituo vyao vya kazi.
Kati ya wakuu wa wilaya wapya 37 walioteuliwa, majina ya
waandishi wa wa habari yemejitokeza katika wateule hao.
Miongoni mwao ni mtangazaji wa muda mrefu wa shirika la
utangazaji nchini TBC, Grace Henry
Kingalame aliyeteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Nyang’halwe mkoani Geita, Kasilda Jeremia Mgeni aliyeteuliwa kuwa
mkuu wa wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro na Jaffar Mohamed Haniu aliyeteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Rungwe
mkoani Mbeya.
Jaffar Mohamed Haniu aliyeteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya. |
Rais ameendelea
kuwaamini Wakuu wa wilaya wenye taaluma ya habari ambao amewahamisha vituo vyao
vya kazi na kuwapeleka maeneo mapya ya
kazi ambao ni pamoja na Godwin Crydon
Gondwe amehamishiwa wilaya ya Bahi mkoani Dodoma akitokea wilaya ya
Kinondoni mkoani Daresalaam, Fatma Almas
Nyangasa aliyehamishiwa kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani
akitokea wilaya ya kigamboni mkoani Daresalaam na Simon Peter Simalenga aliyehamishiwa kuwa mkuu wa wilaya ya Bariadi
akitokea wilaya ya Songwe.
Aidha majina ya wakuu wa wilaya wenye taaluma ya habari ambao
wameachwa katika uteuzi huu mpya ni pamoja na Jerry Muro aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida
ambaye nafasi yake inachukuliwa na Thomas Cornel Apson aliyehamishiwa kutoka
wilaya Siha mkoani Kilimanjaro, na Gabriel
Zakaria aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Busega ambaye nafasi yake inachukuliwa
na Anna Jerome Gidarya aliyehamishiwa kutoka wilaya ya Ileje.
Post a Comment