Meneja wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) Masoud Mrisha akielezea mradi wa ujenzi wa bandari ya nchi kavu mkoani Arusha |
Mwandishi wetu. Arusha.
Bandari ya nchi Kavu inatarajiwa kujengwa katika eneo la King'ori wilayani Arumeru mkoa wa Arusha, ili kurahisha upokeaji na usafirishaji wa mizigo katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini na nje ya nchi.
Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) tayari imeanza upembezi yakinifu wa mradi huo, ambao unakwenda sambamba na ujenzi wa bandari hizo katika maeneo mengine yatano nchini.
Meneja wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) Masoud Mrisha akizungumza na wanahabari |
Akizungumza na waandishi wa habari,Meneja wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) Masoud Mrisha alisema tayari Bodi ya TPA imepitisha mradi huo na ukianza utekelezaji wake inatarajiwa kuongezeka mizigo katika bandari ya Tanga.
"huu mradi utasaidia sana kurahisisha usafirishaji na upokeaji wa shehena ya mizigo kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini na nchi jirani"alisema
Alisema ujenzi wa bandari hiyo ya nchi kavu, unakuja wakati Bandari ya Tanga ipo katika maboresho makubwa ambapo kunatarajiwa kuwepo ongezeko la mizigo kutoka tani 750,000 kwa mwaka hadi tani 3 milioni kwa mwaka.
Mrisha alisema serikali imetoa kiasi cha sh 429.1 bilioni kwa ajili ya maboresho ya bandari hiyo na sasa imeanza kupokea meli kubwa na kupokea mizigo bandari.
Karibu Tawala Mkoa wa Tanga, Pili Mnyema akizungumza na wanahabari. |
Awali Katibu Tawala mkoa wa Tanga,Pili Mnyema aliwataka wafanyabiashara nchini, wakiwepo wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini, kutumia bandari ya Tanga.
Mnyema alisema serikali imetoa fedha nyingi kuifanyia maboresho bandari hiyo,hivyo wafanyabiashara watarajie huduma bora na za kiwango cha kimataifa katika Bandari hiyo.
Meya wa Jiji la Tanga akizungumza na wanahabari juu ya umuhimu wa bandari ya Tanga kwa mikoa ya kaskazini na chi jirani |
Post a Comment