Na Serengeti Media Centre.
Mahakama ya Wilaya ya Serengeti imeridhia Maombi Sita yaliyowasilishwa na mawakili wa Serikali ya kutaifisha na kuuzwa ng’ombe 1772 mali ya wa wakazi wa Loliondo waliokamatwa wakichungia ndani ya Hifadhii ya Taifa ya Serengeti.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya Jacob Ndila,Wakili wa Serikali Nimrod Byamungu Desemba 13 aliwasilisha maombi namba 17,18,19,20,21 na 22/2022 ya kutaka mifugo hiyo itaifishwe na kuwa ya Serikali na kwa sababu utunzwaji wake ni mgumu iliamriwa wauzwe kwa njia ya mnada.
Aliiambia Mahakama hiyo kuwa mifugo hao walikamatwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa tarehe tofauti mwezi huu wamiliki na wachungaji hawakujulikana.
Amebainisha kuwa kosa hilo ni kinyume na Kanuni ya 7 na 20 ya Kanuni za Hifadhi za Taifa,pia ni kinyume na Kifungu cha 18 cha Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori Sura 283.
Hakimu Ndila aliridhia maombi ya ng’ombe hao wanaotajwa kuwa wa wakazi wa vijiji vya Armanie na Mbukeni Loliondo kutaifishwa na watauzwa leo Jumatano Desemba 14,2022 katika Kituo cha Nyabogate kilichoko ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia Kampuni ya Udalali ya Lock site Takers ya Musoma.
Post a Comment