PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: UKWELI WA MGOGORO JUMUIYA HIFADHI WANYAMA BURUNGE (JUHIBU WMA)
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Ofisi ya WMA BURUNGE Mwandishi wetu, Babati   Kwa takriban miezi mitatu sasa kumekuwa na mgogoro katika eneo la hifadhi ya jamii ya wanyamap...
Ofisi ya WMA BURUNGE

Mwandishi wetu, Babati

 

Kwa takriban miezi mitatu sasa kumekuwa na mgogoro katika eneo la hifadhi ya jamii ya wanyamapori ya Burunge(JUHIBU) wilaya ya Babati mkoa Manyara.

 

Mgogoro huo ni kati ya Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Hamis Juma anayeungwa mkono na baadhi ya wajumbe wa baraza la uongozi  na Bodi ya wadhamini wa jumuiya hiyo ambayo inaungwa mkono na baraza la ushauri la maliasili la wilaya hiyo na wananchi waliowengi.

 

Katika mgogoro huo, Juma na wenzake wanataka kuvunjwa mkataba ambao bodi ya jumuiya hiyo lisainii julai 14, mwaka huu na kampuni ya uwindaji wa kitalii ya EBN kuendelea na kitalu hicho wakitaka eneo hilo kupewa kampuni nyingine ya uwindaji.

 

Kutokana na  mgogoro huo, baraza la uongozi la hifadhi hiyo(AA)  hivi karibuni, limetangaza kuifukuza bodi ya wadhamini ya jumuiya hiyo na kumsimamisha kazi Katibu wa jumuiya hiyo,Benson Mwaise.

 

Katibu Wa Jumuiya Benson Mwaise aliyesimamishwa hivi karibuni


Hata hivyo, tayari bodi imepinga uamuzi huo, kwa maelezo baraza la uongozi halina mamlaka kusimamisha bodi kutokana  na hoja ya kutaka kumwingiza kinyume cha taratibu mwekezaji mwingine katika kitalu hicho.

 

Mwenyekiti wa  jumuiya hiyo,Hamis Juma  amekuwa akidai mkataba baina ya JUHIBU na EBN  ni batili kwa hoja ilipaswa kutangazwa zabuni ya kugawa kitalu hicho ili kampuni nyingine ziombe pia lakini pia amekuwa akieleza EBN iliwahi kukiuka taratibu za uwekezaji katika kitalu hicho.

 

Juma pia na baadhi ya wajumbe wamekuwa wakidai mkataba huo, haukuwa shirikishi na ilikiuka taratibu  za umiliki wa vitalu.

 

Hata hivyo,wajumbe wa bodi hiyo, wakiongozwa na mwenyekiti wao, Patricia Mosea  Wamepinga hoja hiyo kwa maelezo kuwa,  EBN hakuwa mwekezaji wa mara ya kwanza (potential/prospective investor) ambaye alitakiwa kwa mujibu wa kanuni ya 55 ya Kanuni za Jumuiya ya Hifadhi za Wanyamapori, 2018 kuingizwa kwenye mchakato wa zabuni/mnada.

“ Kanuni ya 55(10) ya Kanuni za Jumuiya ya Hifadhi za Wanyamapori, 2018 inaweka kigezo cha uhuishaji mkataba kuwa ni alama zitokanazo na taarifa ya tathmini. EBN walipata alama za kutosha kuhuisha mkataba wao na hawakuhitaji kuingizwa kwenye mchakato wa zabuni”alisema Mosea.

 Mjumbe mwingine wa bodi ya wadhamini,  Lebrice Makao alisema  sio kweli kuwa hakukuwa na ushirikishwaji na kuwa EBN ilikiuka tararibu za uwekezaji kama ambavyo Mwenyekiti huyo wa JUBIBU na baadhi ya wafuasi wake wamekuwa wakidai.

 

“EBN walipata uhakikisho wa kuhuishiwa mkataba baada ya Wizara ya Maliasili na Utalii, kufanya  tathmini na mapendekezo ya kuhuishwa mkataba baada ya EBN kupata alama za kutosha kuhuisha mkataba wake”alisema

 

Makao alifafanuwa kuwa   pamoja na EBN kupata alama za kutosha kuhuisha mkataba wake, bado EBN walipitishwa kwenye mchakato mrefu na wa wazi na shirikishi uliochukua zaidi ya miaka miwili kabla ya kuhuishiwa mkataba huo.

 

Makao alisema kuwa,ushirikishwaji ulikuwepo katika kufikia maamuzi ya kusaini mkataba kwani  Baraza la Ushauri la Maliasili Wilaya lilishirikishwa kwenye hatua zote za kuhuisha mkatabalakini pia watendaji wa wizara ya maliasili na Utalii.

 

Alisema Wizara ya Maliasili na Utalii pia  ilishiriki kumfanyia mwekezaji tathmini na kutoa taarifa ya iliyompitisha mwekezaji kuwa ana sifa ya kuhuisha mkataba lakini pia Wizara ilialikwa kushiriki majadiliano na mwekezaji na ilibariki majadiliano yaendelee.

 

“lakini pia  rasimu ya mkataba pia iliwasilishwa wizarani na Wizara kupitisha mkataba huo usainiwe kati ya EBN na JUHIBU sasa tunashangaa sasa kuna watu wapo wizarani wanadai hawakushirikishwa”alisema


BWAWA la MAJI lililochimbwa na kampuni ya EBN hapa Tembo wakiwa wanakunywa maji


 

  Historia ya Kitalu cha  uwindaji cha JUHIBU.

 

Mwaka 2013 Bodi ya hifadhi ya jamii ya wanyamapori Burunge (JUHIBU) ilitangaza mnada wa uwekezaji kwenye kitalu chake cha uwindaji wa kitalii lakini ni mwekezaji mmoja tu, EBN Hunting Safari Limited aliyejitokeza kuwania kitalu hicho

 

 Mnada wa uwekezaji kwenya kitalu cha JUHIBU ulitangazwa kwa mujibu wa kanuni ya 51 ya Kanuni za Jumuiya ya Hifadhi za Wanyamapori za Mwaka, 2012.

 

Bodi ya JUHIBU na EBN waliingia mkataba wa miaka mitano kuanzia 2013 hadi 31 Desemba, 2018 na Mwaka 2017 EBN iliwasilisha maombi ya kuhuisha mkataba wake na Bodi ya JUHIBU.

 

Kwakuwa EBN walikuwa na barua ya Wizara inayoonyesha tathmini ya utendaji wao kuwa walipata alama za kuwawezesha kuhuisha mkataba, JUHIBU iliridhia kuingia mkataba mwingine kampuni ya  EBN kwa kipindi cha miaka mitano mingine kuanzia Januari, 2018 hadi 31 Desemba, 2022.

 

Kigezo kilichotumika kuhuisha mkataba kati ya EBN na JUHIBU kwa miaka mitano ni tathmini ya Wizara iliyoonyesha kuwa utendaji wa EBN ulikuwa wa kuridhisha na kwamba EBN ilipata alama za kutosha kuhuisha mkataba wake. Kutokana na tathmini hiyo iliyotolewa na Wizara, JUHIBU ilitumia kanuni ya 51(10) ya Kanuni za Jumuiya ya Hifadhi za Wanyamapori za 2012 kuhuisha mkataba na EBN.

 

Januari Mwaka 2020 EBN iliwasilisha maombi mengine tena ya kuomba kuhuisha mkataba wake wa uwekezaji kwa muda wa miaka kumi kuanzia Januari 2023 hadi 31 Desemba, 2032.

 

 Maombi hayo ya EBN ya kuhuisha mkataba yaliwasilishwa kwa mujibu wa kanuni ya 55(10) ya Kanuni za Jumuiya ya Hifadhi za Wanyamapori, 2018.

 

 Pia EBN waliomba taarifa ya tathmini ya utendaji wao ili wajue kama wana sifa ya kuhuisha mkataba au lah. Barua ya EBN ya kuomba kuhuisha mkataba ya tarehe 28/01/2020 .

 

 JUHIBU waliomba Wizara iifanye EBN tathmini ili JUHIBU ijue kama EBN wana sifa ya kuhuisha mkataba au la

 

Wizara ya Maliasili na Utalii  iliteua wataalam wanne kufanya tathmini na baadae kutoa baraka

 

Tathmini ilifanywa na wataalam kutoka wizara ya Maliasili na Utalii,  tarehe 26 hadi 29 Juni, 2020 na baada ya tathmini wataalam waliwasilisha taarifa yao wizarani na baadaye iliwasilisha taarifa hiyo JUHIBU  kwa barua ya tarehe 8 Desemba, 2020.

 

Taarifa ya tathmini ya Wizara ilionesha kuwa EBN walipata alama za kuwawezesha kuhuisha mkataba wao wa uwekezaji kwa miaka kumi kama ilivyo kwenye Kanuni za Uwindaji za 2015.

 

Baada ya JUHIBU kupokea taarifa ya tathmini, JUHIBU iliitisha vikao vya wadau na kufanya takriban vikao tisa vya wadau ili kujadili maombi ya EBN ya kuhuisha mkataba na baadaye ilisaini.

 

 

Wizara pia iliarifiwa kuhusu vikao vya kujadili maombi ya EBN na kimsingi Wizara libariki majadiliano na mwekezaji yaendelee.

 

Maafisa  wizara ya Maliasili na serikali walishiriki mchakato.

 

Wajumbe wa vikao vya majadiliano na EBN walitoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Babati, Baraza la Ushauri wa Maliasili Wilaya ya Babati, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, TANAPA, TAWA, JUHIBU, Wizara ya Maliasili na Utalii, Kijiji cha Vilima Vitatu na wadau wengine wa uhifadhi na maendeleo ya jamii wilaya ya Babati.

 

Wajumbe walipitisha azimio kuwa mkataba kati ya JUHIBU na EBN uhuishwe. Kufuatia azimio hilo rasimu ya mkataba uliandaliwa kuhuisha mkataba kati ya EBN na JUHIBU kulingana na kanuni ya 55(10) ya Kanuni za Jumuiya ya Hifadhi za Wanyamapori za 2018.   

 

JUHIBU ilituma rasimu ya mkataba Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ushauri zaidi,

Wizara iliidhinisha mkataba huo usainiwe kati ya EBN na Bodi ya Wadhamini ya JUHIBU. Barua ya JUHIBU kuwasilisha rasimu ya mkataba ya tarehe 20/04/2021 na barua ya majibu ya Wizara kuridhia utiaji sahihi mkataba ya tarehe 26/10/2021.

 

Mkataba kati ya JUHIBU na EBN ulisainiwa julai 14,2022 baada ya taratibu zote za kisheria kufuatwa ikiwa ni pamoja na kuihusisha ofisi yako tangu mwanzo hadi mwisho na kupata baraka zako zote.

 

Huu ndio mgogoro wa uwekezaji katika kitalu cha  JUHIBU WMA , moja na maeneo yaliyopo katika hifadhi ya jamii ya JUHIMU yenye ukubwa wa kilomita za mraba 283 ikiundwa vijiji 10 vilivyopo wilaya ya Babati mkoa wa Manyara.

 

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top