PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: DC ARUMERU AWASISITIZA MADIWANI ARUSHA DC, KUIMARISHA MIKAKATI YA UKUSANYAJI WA MAPATO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango akizungumza kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani, halmashauri ya Arusha wa kujadili ta...

 

Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango akizungumza kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani, halmashauri ya Arusha wa kujadili taarifa za robo ya kwanza ya Julai - Septemba 2022, mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.

Mwenyekiti halmashauri ya Arusha, Mhe. Ojung'u Salekwa akifungua Mkutano wa Baraza la Madiwani wa kujadili taarifa za robo ya kwanza ya Julai - Septemba 2022, mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.

Baadhi Madiwani wakiwa kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani wa kujadili taarifa za robo ya kwanza ya Julai - Septemba 2022, mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.

Baadhi Madiwani wakiwa kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani wa kujadili taarifa za robo ya kwanza ya Julai - Septemba 2022, mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.

Baadhi Wakuu wa Idara na Vitengo, halmashauri ya Arusha wakiwa kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani wa kujadili taarifa za robo ya kwanza ya Julai - Septemba 2022, mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo


Na Elinipa Lupembe.

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango, ametoa salamu kwa wajumbe wa baraza la Madiwani kwa kuushukuru na kuupongeza uongozi wa halmashauri ya Arusha kwa juhudi kubwa zinazofanyika katika kuwahudumia wananchi na kuwasisitiza kuimarisha mikakati ya ukusanyaji wa Mapato.

Akizungumza baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Madiwani la kujadili taarifa za robo ya kwanza cha Julai -Septemba 2022, Mkuu huyo wa wilaya, amewahimiza waheshimiwa Madiwani licha ya juhudi zinazofanyika suala la ukusanyaji wa mapato ni la muhimu zaidi pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapato.

Mkuu huyo wa wilaya ameweka wazi kuwa, ili halmashauri iweze kutimiza mipango na malengo yake, ni lazima ukusanyaji wa mapato ufanyike kwa ufanisi kulingana na makisio ya kibajeti pamoja na kusimamia matumizi ya mapato hayo.

Aidha mhandisi Ruyango, amesisitiza matumizi ya makusanyo yanayozingatia sheria na maelekezo ya serikali ikiwemo asilimia 10 za kwa ajili ya mikopo isiyokuwa na riba kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kama maelekezo ya serikali yanavyoelekeza.

Hata hivyo, mkuu wa wilaya amemsisitiza mkurugenzi wa halmashauri hiyo, kusimamia makusanyo ya mapato hasa kwa mapato yanayokusanywa kwa mashine za POSS kuweka fedha hizo benki kama sheria inaelekeza ya kuwasilisha fedha zote benki mara baada aya kuzikusanya.

Awali amewakumbusha waheshimiwa madiwani, kushiriki katika usimamizi wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao, pamoja na kuwashirikisha wananchi katika usimamizi wa miradi hiyo.

"Halmashauri imepokea fedha kutoka Serikali Kuu,  shilingi milioni 760 za ujenzi wa vyumba 38 vya madarasa kwa shule 15 za sekondari kwa ajili ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka wa masomo 2023, hivyo kila aliyepewa dhamana ahakikishe anashiriki kikamilifu kusimamia miradi hiyo kwa mujibu wa sheria".Amesisitiza Mkuu wa wilaya .

Aidha amaemuagiza Mkurugenzi wa halmashauri kutoa taarifa kwa viongozi wa ngazi zote ikiwemo Madiwani, za miradi yote inaokwenda kutekelezwa  kwenye maeneo yao ya kata, vijiji na vitongoji, ili viongozi wote washiriki katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Waheshimiwa Madiwani, mnatakiwa kufanya mipango ya kuhamasisha wanafunzi wanapata chakula cha mchana wawapo shuleni na kuwahasisha wazazi kuchangia changia chakula cha mchana kwa shule za kutwa

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top