PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: ANGONET WAZINDUA MRADI WA UHIFADHI MAZINGIRA NA KUKUZA UTALII WA ASILI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
 Mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoani Arusha ANGONET wametakiwa kuwa na mpango mkakati ya kuwawezesha mashirika kufanya kazi Kwa...






 Mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoani Arusha ANGONET wametakiwa kuwa na mpango mkakati ya kuwawezesha mashirika kufanya kazi Kwa kuzingatia Sheria za nchi.


 Afisa Maendeleo mkoa wa Arusha Bi. Blandina Nkini amesema hayo wakati wa uzinduzi wa mradi wa uhifadhi wa mazingira na uwezeshaji jamii, unaotekelezwa na mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoani Arusha ANGONET hivi karibu.

Amesema Mashirika mengi yamekuwa yakisigana na serikali Kwa kutofuata utaratibu mzuri uliowekwa na serikali na hivyo kusuguana na serikali wakati serikali inatambua umuhimu wa mashirika hayo Kwa Maendeleo ya jamii.

Aidha amegusia athari wanazokutana nazo watoto wa kiume ambao wapo hatarini zaidi Kwa sasa Kwa kutendewa vitendo visivyo vya kimaadili na kuharibu kizazi kijacho kisichowajibika ipasavyo kulea familia na kuwataka ANGONET kuhakikisha wanakuja na mkakati imara wa kusaidia watoto wa kiume.

Mwenyekiti wa ANGONET Bi. Catherine Baguzu amesema kuwa lengo la mradi huo ni kujenga mahusiano chanya kati ya Rasilimali na jamii inayozunguka Rasilimali kunufaika Moja Kwa Moja na uwepo wa Rasilimali hizo.

Amesema mradi huo wenye kauli mbiu kujali Dunia, kujali watu na mgao sawia unadhamimiwa na  shirika la Maendeleo la umoja wa mataifa UNDP na kuratibiwa na jumuiko la Maliasili nchini Tanzania TNRF, unaotekelezwa katika wilaya za karatu, Monduli na Ngorongoro Mkoani Arusha.

Ameainisha kuwa mradi huo utafanya kazi na vikundi kumi vya ujasiriamali Toka jamii za PEMBEZONI  na kati ya hivyo saba ni vya wanawake, pia Kilimo biashara kwa wakulima 40 na wafugaji 20 ili kubadili mtazamo Kwa wakulima hao wasiwe chanzo Cha uharibifu wa mazingira.

Mratibu wa shirika la ANGONET Bwana Petro Aham amesema mradi huo utachochoea Utalii wa asili, uhifadhi na utawala wa mazingira Kwa kuwafundisha viongozi vijiji na Kata ili kujenga uongozi Bora unaotunza mazingira hayo.

Judith Kimkoki Toka TNRF amesema wao kama waratibu wa miradi hii Kwa taasisi 12 zinazotekeleza miradi hii ya UNDP, wanaipongeza ANGONET kupata mradi huo na waitumie vema Kwani ndiyo nafasi pekee wezeshi Kwa mashirika haya kukua kitaifa na kimataifa

Esupati Laizer Toka Kijiji Cha Selela amesema wamenufaika sana miradi inayotekelezwa na Maipac na CILAO na kuahidi pia kutoa ushirikiano Kwa ANGONET watakapoanza utekelezaji wa mradi huu katika maeneo yao.

Nao viongozi wa halmashauri za Karatu, Monduli na Ngorongoro wameahidi kushirikiana vema na ANGONET katika kutekeleza mradi wa uhifadhi wa mazingira na uwezeshaji wa jamii ili lengo la mradi huo liweze kutumia vema Kwa manufaa ya wakazi wa maeneo hayo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top