PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: SABABU ZILIZOIFANYA MAMLAKA YA HIFADHI NGORONGORO KUVUNJA REKODI YA MAKUSANYO NA KUTOA GAWIO KUBWA SERIKALINI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,Dk Freddy Manongi akizungumza na wanahabari ofisini kwake jijini Arusha mapema leo ju...

Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,Dk Freddy Manongi akizungumza na wanahabari ofisini kwake jijini Arusha mapema leo juu ya mafanikio na mipango ya hifadhi ya ngorongoro kulia kwake ni Dk Msuha naibu mhifadhi wa mamlaka hiyo

Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro, Dk Freddy Manongi akizungumza na wanahabari ofisini kwake jijini Arusha mapema leo juu ya mafanikio na mipango ya hifadhi ya ngorongoro kulia kwake ni Dk. Msuha naibu mhifadhi wa mamlaka hiyo

Baadhi ya waandishi wa habari waliojitokeza kuchukua habari wakimsikiliza kwa makini mhifadhi mkuu NCAA  Dr. Manongi alipokuwa akiwasilisha kwao mikakati iliyowawezesha kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato katika mamlaka ya hifadhi hiyo

Baadhi ya wanahabari mkoani hapa wakiwajibika kazini

Baadhi ya wanahabari hao wakiwajibika kazini

Baadhi ya wanahabari hao wakimsikiliza kwa makini mhifadhi mkuu huyo

NA: ANDREA NGOBOLE, ARUSHA

Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro(NCAA) inatarajia kutumia kiasi cha shilingi bilioni 15 kwa kwa ajili ya ujenzi wa makumbusho ya utalii wa Miamba(jiolojia) ili kuongeza  vivutio vya utalii katika hifadhi hiyo na kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea hifadhini.

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake mapema leo Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,Dk Freddy Manongi, amesema kuwa mamlaka hiyo imefanya vizuri katika ongezeko la wageni wanaotembelea hifadhi hiyo na kuongeza mapato ndani ya miaka mitatu hali iliyowawezesha kutoa gawio kwa serikali zaidi ya lengo walilowekewa.

Dk Manongi amesema katika kuendeleza mapato kwa mamlaka hiyo imeona vema kujenga makumbusho hayo ambayo pia imepata  msaada kutoka serikali ya China, makumbusho hayo yakikamilika kujengwa kutaongeza watalii zaidi katika hifadhi hiyo na kuongeza mapato zaidi ambapo kwa sasa Mamlaka hiyo,inapata wastani wa watalii 600,000 kwa mwaka na wanatarajiwa kuongezeka zaidi kutokana na maboresho yanayoendelea katika Mamlaka hiyo.

Amesema kuwa mapato ya Mamlaka hiyo,yameongezeka kutokana sh 60 bilioni 2014/15 hadi kufikia sh 124 bilioni mwezi June mwaka huu.

Dk Manongi alisema,Mamlaka hiyo pia imeweza kuvuka lengo la kutoa gawio la serikali kutokana sh13 bilioni hadi sh 22.34 billion na kuwa moja ya taasisi za serikali zilizofanya vizuri zaidi katika kuchangia mfuko wa hazina.

Amesema Mamlaka hiyo kwa mwaka huu imeweza kukusanya fedha za ongezeko la thamani(VAT) na kuzipeleka TRA kiasi cha sh 20 bilioni zilizotokana na tozo kwa watalii walioingia hifadhini hapo.

"Mwaka huu pia tumetoa sh 3.4 bilioni kwa wizara ya maliasili na Utalii kama makato ya fedha ya mfuko wa kuendeleza utalii" alisema

Alisema mafanikio haya yametokana na kuboresha mfumo wa makusanyo ya mapato kwa kutumia mfumo wa kielekroniki lakini pia mianya ya upotevu wa mapato imezibwa.

Awali Naibu Mhifadhi wa Ngorongoro ,Dk Maurus Msuha alisema licha ya mafanikio ya kuongeza mapato na kuvutia watalii zaidi pia Mamlaka imeendelea kuboresha maisha ya wenyeji wa Ngorongoro.

Dk Msuha alisema, NCAA imejenga zaidi ya shule 22 katika eneo hilo,imeendelea kutoa msaada wa chakula kwa wenyeji lakini pia imeendelea kutoa msaada ya afya,maji na maendeleo ya jamii.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top