Waandishi wa redio jamii tano Tanzania toka katika mikoa minne ya Arusha,Manyara,Dodoma na Mara walioshiriki katika warsha ya kuwajengea uwezo wa kuandaa vipindi vya kampeni ya kupambana na ukeketaji,ndoa na mimba za utotoni kwenye halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha,ambazo zimeanza kwa mwezi juni wakiwa na mganga wa jadi alimaarufu kama 'Mchawi' katika kijiji cha Sakala wilayani hapo ,Bw.Sangau Naimodu walipomtembelea nyumbani kwake ili kupata maoni yake kuhusu suala hilo la ukeketaji.
Bw Sangau aliwasihi wananchi waliokuwa wamefika kupata huduma nyumbani kwake kuachana na vitendo hivyo ambavyo ni vya unyanyasaji wa kijinsi kwani vimepitwa na wakati ukilinganisha na mfumo wa maisha wa sasa,kwani hata hapo awali hakukuwa na magonjwa kama wakati huu tuliopo, na imegundulika kuwa wakati wa kujifungua wakina mama wengi waliokeketwa wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na kutokwa na damu nyingi,amewaambia kuwa serikali inapiga marufuku ukeketaji na kuendelea kutekeleza hayo ni kosa la jinai na muda wa kuacha umewadia.
Bw Sangau alianza shughuli zake za kiganga akiwa mtoto kwa kurithishwa kwenye ukoo na mababu,na kwa siku moja hupata zaidi ya wateja 20 wenye shida mbalimbali,na huwapa elimu juu ya ukeketaji wakati wanapokuwa wamejikusanya nyumbani kwake, amekiri kuwa magonjwa ambayo hajayapatia ufumbuzi huwaeleza wateja wake na kuwasihi waende hospitalini ili kupata matibabu,amesema ugonjwa wa kifua kikuu,saratani na Ukosefu wa Kinga Mwilini(UKIMWI) ni kati ya magonjwa ambayo hana dawa zake.
Kampeni ambazo zimezinduliwa rasmi siku ya Jumatano wilayani hapa za kupambana na ukeketaji,ndoa na mimba za utotoni zikiwajumuisha wadau mbalimbali pamoja na Jamii ,zinaendelea kwa mwezi Juni ikiwa ni mwendelezo wake kwa miaka mitatu sasa wilayani Ngorongoro na zitaanza rasmi katika mikoa ya Mara,Dodoma na Manyara kwa njia ya redio ambako tatizo hilo limeonekana kuwa kubwa pia,muda huu wa likizo ni wakati ambao vitendo hivyo hufanyika shule zikiwa zimefungwa,shughuli iliyoratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,Sayansi na Utamaduni(UNESCO) wakishirikiana na halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro pamoja na Mtandao wa redio jamii ,Tanzania Development Information OrganAazition(TADIO).
Mwaandishi:Gideon Kiyyian Ole Kiyiapi.
Post a Comment